[wanabidii] JK: Hatutaki kuingiliwa mgogoro na Malawi

Wednesday, November 21, 2012
Wandugu,
Baina ya Mhe Membe na Rais wetu JK tumuamini nani?
Membe katueleza kuwa tumekubaliana kutokukubaliana na Wamalawi na kuwa suala sasa linapelekwa kwa eminent persons wa SADC na kuwa Chinzano wa Msumbiji anaandikiwa.
Rais wetu mpenzi jana Arusha anasema kuwa...."mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi bado unajadiliwa na nchi hizo mbili, hivyo hakuna haja ya mataifa mengine kuingilia."
Rais kaendelea kuwa "...vyombo mbalimbali ikiwamo Sadc, vina wajibu wa msingi wa  kuingilia suala hilo, lakini kwa kuwa Tanzania na Malawi bado wako kwenye meza ya mazungumzo, sasa siyo wakati mwafaka."
 "Malawi na Tanzania bado tuko kwenye mazungumzo, tusingependa nchi au mtu yeyote aingilie kati suala hilo kwa namna yoyote ile, " alisisitiza Rais Kikwete.
Rais Kikwete alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa suala hilo liko mikononi mwa nchi hizo mbili, hivyo ni vyema likaachwa kwanza mazungumzo yaendelee kabla ya kuingiza nguvu ya ziada.

Alisema kwamba Tanzania na Malawi bado zinaangalia ni namna gani ya kuutatua mgogoro huo bila athari kwa pande mbili na kuomba mazungumzo ya amani yaendelee kuchukua mkondo wake."
Suala ni kuwa hivi sasa kwani tumefikia wapi?
Mbona tunababaishwa? Au hilo Ziwa lishauzwa?
Wamalawi wenzetu wameambiwa nini na sisi tunaambiwa nini baada ya huo mkutano wa DSM?
Soma hapa kutoka Nyasa Times:

...bin Issa.

Share this :

Related Posts

0 Comments