[wanabidii] JE KAZI YA MAWAZIRI KUJEINGA CCM

Tuesday, November 27, 2012
Hivi karibuni baada ya kumalizika mkutano mkuu wa CCM Kanali (mstaafu) Kinana amekuwa akizunguka huku na kule akiambatana na mawaziri kufanya siasa yenye nia ya kuijenga CCM. 
Binafsi sina tatizo na Waziri kama yuko likizo akatumia muda wake wa mapumziko kutumikia chama. Ninashawishika ni kinyume cha taratibu za kazi kutumia rasilimali za umma kama magari, posho za safari kutoka serikalini kwa lengo la kutumikia chama.
Nadhani ni vema kazi ya kujenga chama wakaachiwa waajiriwa wa chama watennde kazi hizo.

Nidhamu na kuheshimu kazi na uweledi ni muhimu sana kwa sasa katika jamii yetu sisi Watanzania. 
Hizo kazi za wizarani nani atafanya kama kila waziri akiwa barabarani kujenga chama?
Napendekeza CCM iweke mfumo wa kuigwa na vyama vingine. Hivi mfanyakazi wa umma wa kada ya chini akiacha kazi zake na akitumia gari ya ofisi na rasilimali zingine kufanya kazi za NGO binafsi kwa mfano, na jambo hilo likafanyika bila makubaliano rasmi na bosi wake ataangaliwa tu aendelee au atawajibishwa?Jibu liko wazi atawajibishwa.
Ifikie mahali mawaziri wawajibike kwa umma kwa kuwa wanalipwa kwa kodi zetu na hawalipwi na CCM

Rai yangu ni kuwataka mawaziri na watumishi wengine wa umma tuwatumikie Watanzania kwa nidhamu na unyenyekevu kwa kuwa si wote wanafurahishwa na porojo za majukwaani. watu wanataka kuona kazi zinafanyika zinazoleta tija katika jamii.

Nawasilisha.



Share this :

Related Posts

0 Comments