[wanabidii] MWANDISHI WA HABARI WA NIPASHE AZIKWA

Thursday, October 18, 2012

ALIYEKUWA Mwandishi wa Habari wa NIPASHE, marehemu Vicky Macha (37) amezikwa jana mkoani Kilimanjaro.

 

Vick alifariki Oktoba 14, katika Hospitali  ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Kabla ya mauti kumkuta aliugua ghafla kwa ugonjwa wa malaria na kisukari ambapo alipelekwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu.

Marehemu Vicky alizaliwa Februari 19, 1972 katika kijiji cha Ururau wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro. Ameacha mume na watoto wawili.

Marehemu alianza kuandikia gazeti la NIPASHE linalomilikiwa na kampuni ya The Gauradian Limited mwaka 2009 na kabla ya hapo alikuwa akiandikia gazeti la Majira.

 

Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi-AMINA

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments