Kumetokea wafanyabiashara toka nchi mbalimbali zilizowekewa vikwazo
mbalimbali na umoja wa mataifa kutaka kufanya biashara na baadhi ya
raia wa watanzania kwa sharti la kutumika kwa bendera ya Tanzania
katika biashara hizo , biashara zenyewe ni kati ya Tanzania na nchi
hizo .
Kwakuwa nchi hizi zimewekewa vikwazo sasa zinatumia wananchi wao
kutafuta masoko na fursa nyingine nje ya mipaka yao kinyume na sheria
za kimataifa na mikataba mingine ya kimataifa inayohusiana na
biashara .
Ni vizuri watanzania wawe makini na mitego hii maana hata wao wenyewe
binafsi wafanyabiashara wanaweza kuwekewa vikwazo au hata mali zao
kushikiliwa na mbaya zaidi ni nchi yetu kuingia kwenye matatizo na
mataifa mengine tunayoshirikiana nayo kwa njia moja au nyingine .
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 Comments