KONGAMANO KUBWA LA WANAHARAKATI KUPINGA MAUAJI YA RAIA NA UHURU WA HABARI
Wanamtandao wa kutetea haki za Binaadamu yaani Human Rights Defenders Coalition(THRD).Kwa kushirikiana na Mashirika mengine wakiwemo FemAct ,GDSS,wadau wa sekta ya habari, viongozi wa kiroho yaani masheikh mapadri na wachungaji , wanasheria na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu na wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT), wameandaa kongamano la masaa matatu (saa 4 asubuhi –saa 7 mchana). Kongamano hilo litafanyika Jumatano katika viwanja vya TGNP tarehe 12 Septemba 2012.
Kama sehemu ya harakati zetu za kutetea haki za raia na haki za binadamu kwa ujumla tuomba ushiriki wa kila moja wetu tuunganishe nguvu ili kudai uwajibikaji kwa wahusika.
-
0 Comments