[wanabidii] Wakazi wa Bonyokwa tunahitaji msaada wa kutengenezewa barabara

Friday, August 24, 2012
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kimara, barabara ya kwenda Bonyokwa kuanzia eneo la Kimara Mwisho ina hali mbaya sana.
 
Kwa kuwa nafahamu serikali yetu haina pesa za kugharimia huduma muhimu za jamii niko tayari kuwahamasisha wenzangu tuchange pesa za kununulia dizeli kwa ajili ya greda la kusawazishia barabara hiyo.
 
Kama Mbunge wangu utakuwa umebanwa na majukumu mengi ya Kitaifa, unaweza kumtuma Diwani wetu apite nyumba hadi nyumba kuchukua michango hiyo.  
 
Kama Mheshimiwa Diwani naye atakuwa amebanwa sana, naamini Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu anaweza kutuchangisha pamoja na kuwa anatoka Chama Cha Mapinduzi.  
 
Kama haya yote yatashindikana itabidii umwombe Mama Salma Kikwete atembelee tena eneo letu ili barabara hii itengenezwe usiku na mchana.
 
Tunaomba ulipe umuhimu hili wasije akina Nchemba wakapata la kuongea. Asante sana Mheshimiwa.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments