Mama lishe hana risiti, kinyozi hana risiti, wafanyabiashara sokoni hawana risiti, na makundi mengine mengi hawana risiti. Mwanzoni wafanyabiashara waligomea machine za EFD wakidhani kodi inatozwa kwenye mauzo hapana kodi inatozwa katika faida baada ya kutonga ghara zako za manunuzi.
Sasa tumeelewa ili kuweka kumbukumbu sahihi za biashara, ni kutunza risiti za manunuzi na EFD inakutunzia kumbukumbu za mauzo. hapo kodi halisi inapatikana. TATIZO MAWAKALA WA EFD WANATUUMIZA EFD BEI YAKE NI KUBWA MMNO TSHS.850,000/=.
Kwa nini TRA msianze kutoa TIN number katika chip kama za simu (sim card) ili wauzaji wa EFD machine wawe wengi tuzinunue na kuweka hiyo line yako ya TIN na kuanza kuchapa kazi? mkifanya hivyo hata kinyozi atakuwa na EFD na zitapatikana katika maeneo yetu kama zilivyo simu za mikononi.
Tumuunge mkono rais wetu na tanzania ina wataalamu wa fani hiyo vijana wengi kama wale wa maximalipo na wengine!
TRA mpooooooo
0 Comments