[Mabadiliko] MEENA HII WAIKUMBUKA

Tuesday, August 30, 2016

Uliandika Wanabidii mwaka 2012

Ushahidi, ushahidi, ushahidi,
Kamwe hatutaupata. Hatutaupata kwa sababu katika nchi yetu tuko chini viwango vya Kiafrika.

Jirani zetu Kenya wanaweza kusikia jambo kuhusu rushwa wakachukua hatua kesho yake, wakachunguza hata kama ni Waziri na wakatoa taarifa kwa umma. 

Hapa kwetu ukiandika kuhusu tuhuma jamaa wanasimama kwamba eti kama una ushahidi tuletee. Hata ile level ya taasisi kuwajibisha watuhumiwa kwa sababu za kimaadili haipo.

Ndo maana Mukama, Chiligati na Msekwa wamevuliwa gamba kwa sababu tu walijaribu kuwagusa watuhumiwa wasiogusika. Ukisema rushwa waziwazi ndani ya CCM unageuka kuwa adui wa wengi. 

Jana nilisema kwamba kwamba sijui akina Mangula wataanzia wapi, maana utulivu unaodaiwa kuwa upo ndani ya CCM ni kutokana na watuhumiwa wa ufisadi kuachiwa watambe katika uchaguzi wa ndani ya chama.

Siku wakiguswa tu, mtaniambia. Katika mazingira kama hayo, hatuwezi kusonga mbele. Rushwa na ufisadi ndani ya CCM vimetaasisiwa (instituted corruption) na ndiyo maana maadui wa chama ni wale wanaopinga rushwa. 

Wachapa kazi ndani ya CCM hawatakiwi, ndo maana watu kama Dk Magufuli, Dk Mwakyembe na wengine wenye kasi kama yao, hawapendwi na wengine utendaji wao umewagharimu afya zao. Tony Diallo akiwa Maliasili na Utalii alimgusa Severe akang'olewa.

Kumbe CS Luhanjo aliyekuwa akimlinda Jairo na madudu yake, aliacha mizizi maliasili wakati akiwa KM chini ya Zakia Meghji. Katika mazingira haya, tunawaaminije hawa wapya katika sekretarieti ya CCM? 

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACMr6Qg9qQHf4MM8vYr1JpiRkwHiL9QpA7i4U7qdzxbyzPszhg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments