[Mabadiliko] Ndani Ya Siku Mbili Wana-Iringa Wamechangia Misaada Ya Wahanga Yenye Thamani Ya Milioni Tatu Na Nusu..!

Saturday, February 20, 2016


Ndugu zangu,


Michango mingine ya fedha imetoka kwa wadau wa Mjengwablog kwa kutuma kwa njia ya simu. Jana niliongea kwenye Nuru FM na Ebony FM kuhusu wazo la mtandao huu kukusanya misaada kwa wahanga wa mafuriko Pawaga.

Mwitikio umekuwa wa kunishangaza hata mimi mwenyekiti wenu. Kwa fedha zilizochangwa taslimu na njia ya simu tumeweza hata kununulia magodoro 20. Miongoni mwa vilivyokusanywa kutoka kwa wana-Iringa wasamaria wema ni mahema 9 yenye ubora mkubwa.

Nimevutiwa pia na wanafunzi an viongozi wa Kimarekani kutoka Programu ya CIEE niliokutana nao majuzi ambao nao walipata taarifa hizo na wamechangia shilingi laki tatu fedha taslimu.

Hakika, mwitikio chanya ulilazimu utafutwe usafiri wa lori kwenda Pawaga hiyo kesho.

Shukran za pekee kabisa kwa kijana mwana-Iringa na mtaalamu wa masuala ya transport na logistics, Ahmed Salim ' Asas' ambaye amefanya jitihada za kuhakikisha vilivyokusanywa na wana-Iringa vinafika Pawaga kesho.

Leo, Jumamosi, Feb 20, nitakwenda Pawaga  na kwa vile viongozi wakuu wa Mkoa watakuwa Pawaga, basi, nitakabidhi misaada hiyo kwao ili nao wakabidhi kwa wahusika.

Shukran nyingi kwenu nyote mliounga mkono jitihada hizi na ambao bado mnaendelea kuchangia.

Kwa mwanadamu, kinachoangaliwa ni moyo wako, na si ukubwa wa unachotoa. Hata moyo wako ukiguswa tu kwa yaliyowapata ndugu zetu wa Pawaga ni faraja kwa walioathirika.

Maggid,

Iringa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye6adbO0wP52zQXEbznTx7SF%2Bw8eq7Udx1WFV1hV6QNYxg%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments