1. ZEC yatahadharishwa kasoro uchaguzi Zanzibar..
Hii ni habari kubwa inayopewa nafasi ya kwanza na mtandao wamjengwablog.com.
Tayari wananchi walio wengi visiwani wako katika wakati mgumu kiuchumi na kijamii kutokana na kadhia hii ya kisiasa kutokana na uchaguzi ambao haukwenda vema.
Wazanzibar wanyonge walio wengi hii leo ni walio wagonjwa kiuchumi na wenye kuhitaji tiba ya haraka ili warejeshe matumaini yao. Vijana walo wengi hawana ajira.
Ajira kwa walio wengi inatokana na sekta ya utalii ambayo sasa iko kwenye umahututi kutokana na hofu ya machafuko ya kisiasa.
Kwa hali halisi ilivyo sasa uchaguzi wa marudio ndio mujarab kwa maana ya tiba kwa watu wa visiwani. Wenye kufikiri kususia uchaguzi huo hawawezi kuwa na dhamira ya dhati ya kutaka kuwasaidia Wazanzibar katika hali walizonazo sasa.
Taadhari inayotolewa sasa kwa ZEC kuhusu kurekebisha kasoro za nyuma ndilo jambo, wapenda amani wote tunalopaswa kulihimiza ili tusije tukarudi tulikotoka.
Kama taifa, na kama wazalendo katika nchi tuliyozaliwa na tunayoipenda, tukubaliane, kuwa si kwa maslahi mapana ya nchi yetu, Bara na Visiwani, kutanguliza siasa iliyotawaliwa na uchu wa madaraka uliojengwa kwenye msingi wa maslahi binafsi, kufanya yale yatakayochochea uhasama na chuki zaidi miongoni mwa wananchi wa visiwani.
Na wenye kutaka kutenda dhambi hii, wasije wakashangaa pia watakavyokataliwa na Watanzania walio wengi , wa Bara na Visiwani, wasiopendezwa na matendo yao hayo.
2. Mfumo wa upatikanaji ardhi unakwamisha ' Kilimo Kwanza'
Katika Tanzania kilimo ni moja ya sekta zinazochangia kwenye kutoa ajira. Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Lugimbana anakiri kuwa mfumo wa utoaji wa ardhi hauko sawa. Uwekezaji kwenye kilimo umerudishwa nyuma kutokana na kutokuwepo kwa mifumo inayoeleweka katika kupata maeneo ya ardhi kuwekeza katika kilimo. Ni sababu zipi zinazopelekea hali hiyo? Habari hii ya gazetini haikutoa majibu ya msingi. Hii ni habari yenye kuhusu uchumi na inapewa nafasi ya pili kwa uzito.
3. Mazembe yamgomea Samatta..
Hii ni habari ya kimichezo inayopewa nafasi ya tatu kwa ukubwa na mtandao wa mjengwablog kwa vile ni ya kitaifa pia.
Mbwana Samatta ni jina kubwa Tanzania na Afrika. Kwa kupata nafasi kucheza Ulaya Mbwana Samatta litakuwa ni jina kubwa duniani hususan kwenye medani ya soka. Watanzania wanafuatilia kwa karibu habari za Mbwana Samatta. Taarifa kuwa TP Mazembe kumgomea Samatta kwenda Ubelgiji zitapokewa kwa masikitiko makubwa na Watanzania wapenzi wa soka na hata wasio wapenzi wa soka.
Swali la kujiuliza; Mbwana Samatta amemkosea nini tajiri wa TP Mazembe Moise Katumbi?
Soma habari nyingine nyingi za magazetini. Ni kwenyehttp://mjengwablog.com
Maggid Mjengwa,
Mhariri/ Mchambuzi wa Habari za mtandaoni
Mjengwablog.com/Kwanzajamii
0754 678 252
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments