[Mabadiliko] Habari Kubwa 3 Za Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com....

Saturday, January 23, 2016


1. Jecha atangaza tarehe ya uchaguzi kurudiwa Zanzibar..

Bila shaka yeyote, hii ni habari kubwa inayopewa nafasi ya kwanza kwa uzito na mtandao wa Mjengwablog.com.

Ni habari yenye kuleta matumaini. Tumechambua huko nyuma, kuwa mgogoro wa Zanzibar ni wingu zito lenye kuweza kuleta mvua ya maafa, si visiwani tu, hata bara.

Kama taifa, viongozi waongozwe na hekima ya yalopita si ndwele, tugange yaliopo na yanayokuja mbeleni.

Kwa hali iliyotokea na kupekelekea kufutwa kwa matokeo, na kwa kuzingatia kuwa wapiga kura wa visiwani hawazidi hata laki 5, sisi wa mtandao wamjengwablog.com tuliweka bayana hapa, kuwa hakuna namna nyingine, bali ni kuitafuta busara ya kurudia uchaguzi huo chini ya uangalizi wa karibu wa wasimamizi katika upigaji na uhesabu wa kura.

Na wala tusijitie ujinga kwa kuamini visiwani na bara kutatulia pale, katika mazingira yaliyopelekea kufutwa kwa uchaguzi, leo mmoja katika pande hizo mbili apewe ushindi wa mezani kwa njia ya mdomo.

Ni kupitia sanduku la kura tu, wapiga kura wapewe fursa ya kuchagua. Kwa mpiga kura, alichokichagua mara iliyopita, yumkini atakichagua tena. Na asipofanya hivyo, ni haki yake pia.

Matokeo yakitoka, bado Zanzibar ina utaratibu mzuri wa kikatiba, wa kuundwa kwa Serikali ya Mseto. Na Zanzibar hilo haliepukiki. Tunawatakia kila la heri ndugu zetu wa Zanzibar.

2. Wasomi wataka mchakato wa Katiba uanze upya..

Hii ni habari inayopewa nafasi ya pili kwa uzito na mtandao huu wamjengwablog.com

Suala la Katiba bado linatawala fikra za Watanzania. Na pengine si suala la kuanza upya mchakato, bali ni kuendelea na ulikoishia. Suala la hitaji la uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi linarejewa kila wakati. Kimsingi liko wazi. Ni imani yetu Tume hiyo itapatikana na itasaidia kwenye kuleta amani na utulivu kabla, wakati na baada ya chaguzi zetu.

3. Hali ni mbaya Benki ya damu...

Hii ni habari kubwa pia kwa siku ya leo inayopewa nafasi ya tatu. Inaelezwa , kuwa mahitaji ya damu kwa mwaka ni chupa 450,000 na zinazokusanywa ni chupa 160,000.
Ni dhahiri kuwa hospitali zetu zinahitaji akiba ya kutosha ya damu kuwahudumia wagonjwa wenye kuhitaji. Habari kwamba ukusanyaji wa damu kuwa mdogo kutokana na kutokuwepo kwa wachangiaji damu wa kutosha ni habari mbaya.

Ni wajibu wetu sote kushiriki kuchangia damu kila inapowezekana. Swali kwako msomaji, ni lini mara ya mwisho umechangia damu? Kama hujawahi, ujue hujachelewa. Changia damu okoa maisha ya wanadamu wenzako.

Soma habari nyingine nyingi, ni kwenye http://mjengwablog.com

Maggid Mjengwa
Mhariri/Mchambuzi wa habari za mtandaoni
Mjengwablog.com/KwanzaJamii.com
0754 678 252

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye78Frkt9NJ_Lwpi-oB7eLWk7E6BMGXHTYwbD6H_JF1v-w%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments