Ndugu zangu,
Kuna wakati Mwalimu Nyerere alipata kuulizwa juu ya uwepo wa Wakatoliki wengi kwenye Baraza aliloliunda. Mwalimu alishangazwa na swali hilo, na alijibu, kuwa alichoangalia yeye wakati wa kuunda baraza ni mahitaji ya Watanzania, na hivyo, aliwatafuta wale wenye uwezo na sifa za kufanya kazi itakayokidhi mahitaji ya Wananchi walio wengi.
Tunaona mpaka anapolitangaza Baraza lake, Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli alikuwa bado hajawapata mawaziri wanne wenye uwezo na sifa za kujaza nafasi kwenye wizara nne.
Ni dhahiri, si kila mmoja ataridhika na baraza hilo dogo la mawaziri. Pamoja na ukweli kuwa mamilioni ya Watanzania wameonyesha kulikubali baraza, bado, siku zote, zitajitokeza sauti za wenye kubeza .
Hata hivyo, ni ukweli kuwa , kwa Rais Magufuli kuchukua muda mrefu kufanya tafiti za kina juu ya mahitaji ya Watanzania, na kwa kuangalia uwezo na sifa za atakaowateua, imedhihirisha, kuwa Rais Magufuli alikuwa makini kwenye kuifanya kazi hiyo ya uteuzi.
Ona, uteuzi wa Dr Augustino Mahiga kama Waziri wa Mambo ya Nje. Ni kwa kuangalia hali iliyopo kwenye Ukanda wetu na dunia pia. Kuna changamoto nyingi, ikiwamo ya Ugaidi. Kuna migogoro mingi yenye kuhitaji upatinishi. Tanzania, huko nyuma imekuwa na jukumu la' Kaka Mkubwa' anayefuatwa na mataifa mengine kuombwa ushauri au kuingia kwenye upatanishi kwa migogoro yao. Mtu wa aina ya Augustino Mahiga ni chaguo sahihi la kufanywa Waziri wa Mambo ya Nje mwenye jukumu pia la kuitangaza nchi kimataifa na kuitetea inapobidi. Uwezo na sifa hizo anazo Augustino Mahiga.
Pamoja na kuwa ni Baraza dogo la Wizara 18 na mawaziri 34, lakini, tumeliona Baraza lililo na mchanganyiko wenye siha na linaweza kuwa kama shamba lenye matunda ya aina mbali mbali. Ndio, ni Baraza lenye mawaziri wenye uzoefu mbali mbali na wa vizazi tofauti. Ni mawaziri wanaoweza kujifunza mengi kutoka miongoni mwao. Kujifunza yale yanayoweza kuwasaidia kwenye kazi zao.
Maana, katika mseto huo murua wa Baraza, tunaliona, kuwa ni Baraza lenye, hadi sasa, wanawake saba. Ni Baraza lenye vijana wa kizazi Cha Azimio la Arusha, miongoni mwao ni mawaziri wa aina ya Simbachawene na Hussein Mwinyi. Na kuna mawaziri waliozaliwa baada ya Azimio la Arusha, ni mawaziri wa aina ya Angela Kairuki na January Makamba.
Na kuna mawaziri pia waliozaliwa kabla ya Uhuru, ni mawaziri wa aina ya Charles Mwijage na Harrison Mwakyembe.
Watanzania wanaelewa, kuwa Rais wao Magufuli hakuwa na sababu wala hakupaswa, katika Baraza hilo dogo na la muhimu kwa taifa, kuwateua mawaziri kwa vigezo vya kanda wanazotoka, dini zao, makabila yao au rangi zao. Hilo limemsaidia Rais John Magufuli kutoka na Baraza Dogo la kihistoria kwa kwa na hata Waziri mlemavu wa ngozi.
Kilichotegemewa na ndicho kilichotokea, ni Rais Magufuli kuwateua mawaziri wake kwa kuangalia mahitaji ya Watanzania, kisha , kuwatafuta wenye sifa na uwezo wa kutekeleza yale ambayo Watanzania wanayataka kwa maendeleo yao. Na katika hilo la mwisho, Watanzania hawatazami dini, kabila au rangi ya mtu, bali ni Utanzania wa mtu huyo kwa maana ya uzalendo na utendaji wake wa kazi.
Maggid,
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments