[wanabidii] Kubene amekanyaga moto wa Paul Makonda

Tuesday, December 15, 2015
Na Ally Linje
Wadau, amani iwe kwenu.

Inaonekana ama Kubenea hajui majukumu yake ama anatafuta umaarufu katika mambo ambayo hana uwezo nayo.

Tangu achaguliwe kuwa mbunge, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amekuwa kituko nje na ndani ya bunge. Ndani ya Bunge, Saed Kubenea anaonekana mtu wa jazba, chuki, husda na hasira za kijinga. Alinichekesha sana siku ile alipofura na kukataa maneno yake bungeni wakati aliponukuliwa na mbunge wa CCM kuwa alikuwa amefurahia uteuzi wa Rais Magufuli kwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu. Hakika inasikitisha sana kwani wakati anafurahi alikuwa off camera ila akiwa on camera akajifanya kuwa na chuki za kipumbavu.

Nje ya Bunge na hasa jimboni kwake, Kubenea inaonekana kabisa hajui hata aanze na nini. Ameahidi mambo mengi ambayo hana uwezo wa kuyatekeleza. Badala ya kutumia muda huu kukutana na wadau mbalimbali kupanga mikakati ya kutatua kero hizo, yeye anashinda kwenye Ofisi za CHADEMA pale Ufipa Kinondoni na kwenye gazeti lake la Mwanahalisi kutunga uongo ili mradi tu ajipatie fedha. Kubenea ameshindwa hata kuandaa ziara za kujitambulisha kwenye kata ili kutoa shukrani kwa waliomchagua na kukaa nao kwa karibu ili kuweka mikakati ya kutatua kero zao. Kubenea hajafanya hivyo.

Sasa anaingilia mambo ambayo hana uwezo nayo. Kusuluhisha migogoro baina ya Wafanyakazi na Mwajiri. Mbaya zaidi, anasimama upande mmoja na hivyo kuchochea zaidi mgogoro badala ya kusuluhisha. Big up sana kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda kwa approach nzuri anazofanya ambazo zimepelekea kutatuliwa kwa migogoro mingi kama vile mgogoro wa Madereva wa mabasi na mgogoro wa wafanyakazi wa kiwanda cha Urafiki.

Huko mitaani, wananchi wanaendelea kulalamika huku wakijilaumu kwa kuchagua mbunge mzigo. Wanasikika wakisema kuwa Wana Ubungo wameuziwa mbuzi kwenye gitaa kwani Kubenea aliyekuwa anasifiwa na viongozi wa CHADEMA halingani na huyu Original. Wamechoka na wameshamchoka kiumbe huyo na hawataki hata kumuona.

hisani ya Jf

Share this :

Related Posts

0 Comments