Ndugu zangu,
John Magufuli anaogelea sasa kwenye mawimbi ya mafanikio ya kupigiwa mfano kwenye utawala wake. Hata hivyo, kuna kila dalili pia, kuwa wakosoaji wa John Magufuli nao wamejipanga kwenye kuona namna atakavyowachagua mawaziri wake na hata muundo mzima kwa ujumla wake.
Kama ni mchezo wa kuruka kamba, Magufuli ameshaweka kipimo cha kamba. Ameonyesha dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi, hivyo, haitarajiwi, kuwa miongoni mwa Mawaziri wake waonekane ni wenye makandokando ya ufisadi.
Bila shaka, Magufuli kwa sasa anapitia taarifa zote muhimu kwa anaokusudia kuwateua, maana, kwa kiwango alichokiweka Magufuli, akimteua, mathalan, Waziri atakayebainika kuwa ana biashara zake kubwa za binafsi au hata hisa kwenye biashara kubwa za wengine, huyo, atapunguza ama kuondoa kabisa uhalali wa Serikali ya Magufuli kudai inapambana na ufisadi, maana, ni lazima Waziri huyo achague kati ya uongozi wa kisiasa na biashara zake kubwa.
Na baya kabisa, ni pale itakapotokea, Magufuli amemteua Waziri na ikabainika baadae kuwa Waziri huyo amekwepa kulipa kodi kwenye biashara zake binafsi kubwa.
Yumkini ndio sababu inasemwa Magufuli amewaandalia mikataba mawaziri hao, huenda kukawa na kipengere cha mkataba kinachosema, ' Ukikutwa na kashfa yeyote ile yenye ushahidi wa vielelezo, usisubiri nikufukuze kazi, ondoka mwenyewe!'
Kwa kasi na kiwango alichokiweka Magufuli, yawezekana kuna Waziri atakayeteuliwa na kuvunja rekodi ya kubaki kazini kwa kipindi kifupi sana katika historia ya nchi, maana, hata akihamishia mali zake kwenye majina ya ndugu zake itafahamika tu, na atasakamwa, na wakosoaji wa Magufuli.
Naam, wakosoaji wa Magufuli nao watayafanya hayo, ya kuibua madudu ya mawaziri wa Magufuli ambayo Magufuli mwenyewe hakuyabaini na huku wakitamka ' Hapa Kazi Tu!'
Maggid,
Iringa.
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye4Q2d54R_F1iaNVddrDmb_czC3DZbY6HUxfMkBC8gudrQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments