[Mabadiliko] Habari Kubwa Tatu Leo Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa Mjengwablog.com

Tuesday, December 22, 2015


1. Mikataba ya Wastaafu sasa basi.
Ni habari iliyopewa nafasi ya kwanza na Mjengwablog.com. Ni hatua sahihi kuhakikisha kuwa wastaafu wanatoa nafasi kwa wengine. Ni kwa vile pia, Serikali ilishaandaa mipango ya kurithisha majukumu. Inavyoonekana, kuna baadhi ya watumishi huwa hawajiandai kustaafu na hivyo kufanya idara nyingi za Serikali kuongozwa na akina ' Nkurunziza'. Wale wasiotaka kung'atuka.

2. Kagame amvulia kofia John Pombe Magufuli
Ni habari ya pili kwa ukubwa kwa mujibu wa Mjengwablog.com. Inahusu kutambuliwa kwa jitihada za Serikali ya John Magufuli za kupambana na ' panya' wa bandarini ambao pia wameathiri uchumi wa nchi jirani kama Rwanda yenye kuitegemea bandari ya Dar. Bandari ni kiungo muhimu. Inasemwa, kuna wakati Kagame alipata kutamka, kuwa Tanzania ingempa mkataba wa kuendesha bandari japo kwa muda mfupi, basi, wangeiona tofauti. Soma habari hii yote iliyoshika nafasi ya pili kwenyehttp://mjengwablog.com

3. Polisi Moshi wamkamata mlinzi wa Mfalme wa Qatar. Amekutwa na fuvu la kichwa cha twiga. Alikuwa analipeleka wapi, kwa mfalme? Ni habari iliyochukua nafasi ya tatu kwa ukubwa kwa mujibu wa Mjengwablog,.com. Isome habari hii na nyingine zote ikiwamo habari namba moja ya michezo na katuni bora ya leo na kwenye http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at https://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye6PUS%3DpU4guWxcNJUZ_6oAUro_Svn%3DX3xsPQOTjvev6XA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments