[wanabidii] Maswali 3 au 4 ya Ugomvi: Kwa Wanaomlilia Maalim Seif...

Friday, November 20, 2015

Maswali 3 au 4 ya Ugomvi: Kwa Wanaomlilia Maalim Seif...

Swali la Ijumaa: Nimeona na kusikia kundi la wabunge wakiimba "Maalim Seif, Maalim Seif". Na nimesoma hoja nyingi za kutaka Seif atangazwe mshindi. Hadi hivi sasa sijapata majibu ya kuridhisha na naomba mwenye nayo atusaidie:
1. Wanajuaje Seif kashinda Uchaguzi wa Zanzibar?
2. Kwanini Wanaamini hiyo sababu ya kuwa Seif kashinda?
3. Kwanini wanafikiri ukomo wa Rais wa Zanzibar ni siku yake ya kuapishwa (yaani miaka mitano kamili tangu alipoapishwa)?
4. Kwanini hawakumlilia Lowassa mbele ya Magufuli ambaye naye inadaiwa amepora ushindi na badala yake wamemlilia Seif mbele ya Shein wakati Shein hajatangazwa mshindi au kudai kushinda? Walimfanyia Kikwete kwa sababu waliamini kapora ushindi wa Slaa. Siyo kwamba kwa kutomlilia Lowassa mbele ya Magufuli wamethibitisha kuwa wanamtambua kuwa ni mshindi halali na madai ya Lowassa kuwa ni mshindi hayakuwa na msingi wowote katika ukweli?

Share this :

Related Posts

0 Comments