Ndugu zangu,
Katika kitabu chake; The Flags Changed At Midnight- Mwandishi na ambaye alikuwa DC wa Mkoloni kuanzia 1951-62, Bw. Michael Longford anaelezea jinsi Serikali ya Mwingereza ilivyokuwa makini.
Anasema, kuwa aliyethubutu kuchezea shilingi ya Serikali alijuta kuzaliwa.
Naam, Serikali ya Magufuli imeshaingia, na kasi yake. Umma umechoka na vichwa vya habari, vya mathalan; "Mamilioni yametafunwa halmshauri fulani!'
Maana, kuna walioishi wakiamini, kuwa ng'ombe wa Serikali huzikwa na ngozi yake. Ni nani anayejali? Maana, kama ng'ombe ni wa mtu binafsi, basi, akifa, atahakikisha walau anachuna ngozi yake, ili walau aambulie senti kidogo! Utamaduni huu wa kudhibiti mapato ya hazina ni utamaduni mwema utakaomsaidia mwananchi wa kawaida.
Na liwe Neno La Leo.
Maggid ,
Iringa
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye4RVg9wbdeD%2B1SyjNxL0ZdO%3DSLzYdh3GddK15jnPTyq1Q%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments