[wanabidii] Kwanini Dk. Magufuli na si Lowassa?

Saturday, October 24, 2015
Kwanini Dk. Magufuli na si Lowassa?

Baada ya kuwapima na kuamua, kwa vigezo kabisa vinavyoendana na historia ya Taifa hili, ndiyo maana sisi wengine tunawashawishi watanzania wenzetu, wasomi, vijana kwa watu wazima na wazee kina mama na kina baba wasaidie kulinda heshima ya taifa lao kwa kumkabidhi nchi Dk. Magufuli na si mwingine.

Kwanini Dk. Magufuli na si Lowassa? Ni mchapa kazi, fuatiliaji na wanaosimamia maamuzi magumu yenye maslahi mapana kwa wananchi wake. Hilo halina Ubishi Kabisa.

Tunamuhitaji Dk . Magufuli kwa kuwa anaweza akakurushwa na
usiku w manane akapanda chop na kukagua mlima Kilimanjaro hata usiku wa Manane, na kupanda hadi juu kabisa kileleni akizunguuka akijua kuna moto unawake au kwa nini barafu imeyeyuka.

Tunamuhitaji Dr. Magufuli kuliko Lowassa kwa kuwa anaweza kuwahutubia wana jumuia ya Harvard nchi marekani au jumuiya ya oxford cha uingereza kwa saa mbili wakati Lowassa hawezi kwa jinsi anavyoonekana.

Lakini hata kwa kupima nia na dhamira ya Dr. Magufuli na Lowassa katika nafasi hiyo ya urais wa Tanzania. Dk Magufuli anaonyesha na dhamira na nia ya kweli kutaka kuwatumikia watanzania wakati Lowassa anonekana akitafuta fursa ya kujiongezea utajiri wake. Ukweli utatuweka huru.

Kwanini nasema Dk. Magufuri anaonekana na dhamira na nia ya kweli kutoka moyoni ya kutka kuwatumikia watanzania na Lowassa, anaoneka na nia na dhamira ya kuongeza fursa tu?

Dk. Magufuli anayo ridhaa bya asilimia 100 ya chama chake kugombea nafasi hiyo na kote anakokwenda ananadi ilani ya chama chake na kutoa ahadi zinazotambuliwa na chama chake kutokana na Ilani hiyo.

Lakini Lowassa ameitafuta nafasi hiyo kwa nguvu ya pesa na si kwa ridhaa ya chadema, pili hana ilani mkononi ya chama chake, hivyo anayoahidi yote hayatambuliwi na chma ambacho kesho kitakuja kuulizwa na wananchi.

Watanzania tusidanganyike tuchukue hatua ya kuwakata wote wasio na nia na dhamira ya kweli ya kututumikia kuanzia wabunge na madiwani pia tuwakate wote wasiofanana na Dk. Magufuli katika kupambana na Rushwa na ufisadi wakiwemo wabunge na madiwani. Bila kuwasahau mafisadi wengine ambao bado hawajatoka ndani ya ccm tuwakate tu bila ya huruma ila kumpa kazi nyepesi Magufuli ya kuwashughuliukia

Share this :

Related Posts

0 Comments