Kila mtanzania mwenye ufahamu wake anafahamu kwamba , tangu enzi za Mwl. Nyerere hadi sasa, Mataifa makubwa duniani, yanapotaka kufanya jambo lolote linalohusu bara la Africa lazima kwanza yaulize Tanzania kupata msimamo katika jambo hilo ambalo mataifa makubwa duniani yanataka kufanya.
Hiyo ndiyo Tanzania ya jana, leo na kesho. Taifa lisiloyumba kwa namana yeyote ile, linaokuja suala zima linalohusu utu wa mwanadamu, amani, umoja na mshikamano. Taifa amabalo kiongozi wake anapokuwa kwenye vikao vya kimataifa kila mkuu wan chi anatamani kusikia Tanzania inasema nini katika jambo Fulani lililoko mezani.
Kwahiyo suala la kumtafuta raisi wa Tanzania kamwe haliwezi kufanyiwa mzaha. Tunamtafuta rais wa Tanzania ambaye ni alama kuu ya Africa, ni alama kuu ya dunia.
Rais wa kwanza ni taswira bya nchi yetu anapokuwa ndani ya nchi na nje ya mipaka yetu. Hatumchagu rais wa kujifungia magogoni bali rais amabaye atakayekuwa alama ya Tanzania popote atakakapokwenda, iwe nchi za mataifa makubwa kama Marekani na China, lakini hata katika vinchi vidogo vya Monaco, Malta na Grenada.
Tunamfuta rais Ambaye akisimama baraza la umoja wa mataifa, anaweza kulihyutubia hata siku nzima na asitoke hata mjumbe mmoja kutoka nje ya ukumbi kwa lengo kujisaidia haja ndogo kwa sababu historia hiyo ipo nchi hii.
Ni kwa sababu ya historia hiyo, pamoja na heshima ya pekee duniani ambayo taifa hili limebahatika kuwa nayo, ndiyo maana karibu mataifa yote ya duniani yanayoendeshwa kwa misingi ya demokrsia, imetuma wawakilishi wake kuja
Tanzania kushuhudia kwa macho uchaguzoi mkuu.
Inabidi wje kwa wingi kuona jinsi kuona jinsi watanzania weatakavyofanya maamuzi ya kuamua hatma ya taifa lao. Kuona kama baada ya October 25 itabaki kuwa Tanzania ile ile iliyosisiw na Mwl Nyerere au itzaliwa uya Tnzania nyingine.
Kwa hiyo sisi wwengine baada ya kuwapima wagombea wote hao nane ambao ni lazima kama Taifa Tumpate mmoja wao, Kwa maana Dr. Magufuli na Lowassa kwa kuangalia yote hayo ya jana leo na kesho tunasema Mgufuri ni Zaidi ya Lowassa.
Narudia tena kwa kusema October 25 ni ya Magufuli kwa kuwa atatufikisha tunapotaka kwenda, pia Magufuli alinda hadhi yetu kimataifa na kuendelea kuiba haiba Tanzania katika ulimwengu wa siasa na demokrasia duniani kote
Watanzani Tusifanye Makosa ya kuivunjia heshima nchi yetu kitaifa na kimataifa , Hatuitaji rais amabaye anaulizwa atapambanaje na ufisadi anasema aanaulizwa swali gumu, Hatumtaki rais amabaye anaulizwa maswali na vyombo vya habari vya kimataifa nasema anamtupia shutuma mwandishi kuwa anamuonea.
Chagua John Pombe Magufuli Kwa Tanzania ya jana leo na kesho.
0 Comments