[wanabidii] Double Standards Katika Siasa Zinatugharimu na Zitatugharimu Sana!

Wednesday, October 28, 2015

Kuna double standards nyingi ndani ya nchi moja...

1. UKAWA (yenye CUF ndani) + CUF original ya Zanzibar (isiyo na UKAWA ndani)

2. Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  (yenye Zanzibar ndani) +
Zanzibar original (yenye katiba na serikali yake kamili)

3. Tume mbili za Uchaguzi NEC + ZEC huku moja ikifanya kazi za Zanzibar tu lakini madhara yake yanaiathiri NEC ya JMT.

4. Chama kimoja kuongoza serikali 2 tofauti... Hili ni bomu endapo chama kitashinda ama kushindwa upande mmoja.... na ni changamoto kwa vyama vinavyofuata mfumo huu...
hasa pale kulazimishwa kuwa na wafuasi au wanachama pande zote.. huwezi kuwa na uhakika wa chama kushinda chaguzi zote Jamhuri na Zanzibar. Matokeo yake ndio kujikuta una vyama 2 ndani ya nchi moja kimoja kikiongoza upande wa Zanzibar tu huku kingine kikiongoza JMT.

5. Tumekuwa tukiishi kwa mazoea ya Ilani moja kuongoza serikali mbili zinazotawaliwa na chama Kimoja bila kufikiri kinyume chake!

6. Hakuna Chama chochote cha siasa chenye uhakika wa kuongoza serikali zote mbili ukiindoa CCM ambayo ina favour ya kuwa chama pekee muda mrefu. Chama kikiundwa Zanzibar kinaweza kufanikiwa kuongoza huko huko Zanzibar km CUF lakini hakiwezi Pata majority vote Bara. Kadhalika kikiundwa bara kinaweza kupata ridhaa ya Kuongoza JMT lakini kikakosa wafuasi Zanzibar. Ni Utata tu.

Waasisi wa Taifa hili waliliona na ndio maana walivunja vyama na kuunda chama Kimoja tu kuondoka mikanganyo na utata wa namna hii. Hii haiwezi kuwa valid kwa mazingira ya vyama vingi vya siasa katika nchi ambayo bado pia ina utata wa idadi ya Serikali zinazotawala kama Tanzania.

Hilike ni bomu kubwa na katiba inapaswa ilitazame kwa macho mapana....

Ama tuwe fair kwa serikali 3.. Zanzibar, Bara na Serikali ya Muungano au Serikali moja tu across kuondoa hizi sintofahamu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments