[Mabadiliko] Tukumbushane: Kutoka UDETA Hadi UKAWA...

Tuesday, October 20, 2015


Ndugu zangu,

Nimekuwa nikihimiza kuwa historia ni mwalimu mzuri, na kwamba , ili wanadamu tuweze kuelewa kinachotokea leo, na hata kuweza kubashiri kitakachotokea kesho, hatuna budi kujitahidi kukumbuka kilichotokea jana, hivyo, umuhimu wa historia.

Katikati ya mijadala ya leo, yumkini baadhi ya wajumbe wangu mlikuwa wadogo sana tunapozungumzia miaka ya mwanzoni mwa siasa za mageuzi hapa nchini, lakini, umri hautuzuii kujifunza kilichotokea kupitia kusoma historia, au kupitia simulizi.

Mwaka 1995 utabaki kuwa ni wa kihistoria kwa matukio yake. Nakumbuka, mwanzoni kabisa mwa 1995 zilianza dalili za mgogoro wa ndani ya chama ndani ya NCCR. Mwenyekiti Mabere Marando hakuelewana na Katibu Mkuu Prince Bagenda. Ilinong'onwa mitaani wakati ule, ugomvi wao ulikuwa wa tofauti zao za kibinafsi na kulikuwa na harufu ya ukabila pia. Prince Bagenda na Marando bado wako hai na ni wakati kwa wachambuzi kuwatafuta watu hawa kutoa reflections zao za matukio ya wakati ule.

Tofauti zao zikapelekea hata chama kugawanyika; kukawa na NCCR- Mageuzi ya Mabere Marando na NCCR-Asilia ya Prince Bagenda. Ni NCCR- Mageuzi iliyoanzisha majadiliano na Chadema ili kuunda umoja wao ambao ungejulikana kama - Umoja wa Demokrasia Tanzania- UDETA. Jambo hili likaja kuzimika pale Augustine Mrema alipotoka CCM na kujiunga na NCCR Mageuzi na Marando aliuona ' mtaji' ule mkubwa wa kisiasa na akawa tayari kuachia nafasi yake ya uenyekiti na kumpa Mrema. Hii nayo ni rejea muhimu katika kurutubisha mjadala wetu...
Maggid,

Iringa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye5fAmpeC4x2FWecqSJe0kd13gBbzzMrQjSD0p9LmUd2wA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments