[Mabadiliko] Neno La Leo: Mabadiliko

Friday, October 30, 2015


Ndugu zangu,

Uchaguzi umeshapita. Tunafungua sasa ukurasa mwingine. Lakini, haina maana ya kuacha kufanya tathmini yakinifu ili tuweze kujifunza.

Tumeona, kuwa dhana ya mabadiliko ilitawala uchaguzi wa mwaka huu. Ni sahihi, kuwa mwanadamu, kwa asili, ni kiumbe mwenye kutamani mabadiliko. Ni kuanzia kwenye mavazi, chakula na mengineyo.

Tumekuwa wavivu sana wa kutafakari kwa kina juu ya tunamaanisha nini tunaposema tunataka mabadiliko katika nchi. Bahati mbaya, baadhi ya wanasiasa wameonyesha udhaifu mkubwa katika kuielewa dhana ya mabadiliko, ikawa kama wimbo wa taarab tu.

Ikafika mbali, kuwa waliosimama majukwaani kuhubiri mabadiliko hawakujua kama walifanya kazi pia ya kumhujumu mgombea ama wagombea wao wenyewe.

Sifa moja kubwa ya Watanzania ni dhamira na utayari wao wa kukataa kudharauliwa. Ilipofika mahali, watu wazima wanaojiita viongozi wakasimama majukwaani na kutamka; " CCM imechoka, nendeni mkachague hata jiwe!"

Huko ni kuwadharau Watanzania. Ni kauli kama hiyo ndio iliyowafanya Watanzania wengi waviache vitanda vyao alfajiri na mapema siku ya Uchaguzi Mkuu, waende kuhakikisha wanazuia 'mawe' yasipite. Maana, haikuwaingia akilini kuwa kwa miaka 54 CCM haikufanya chochote na kwamba imefika wakati wa kufanya mabadiliko kwa kuyaweka ' mawe' na CCM kuichimbia shimo kabisa. Kwenye siasa kauli zinaweza kupelekea kupanda au kuanguka kwa chama na mwanasiasa.

Na tuendelee kuitafakari dhana ya mabadiliko.

Ni Neno La Leo.

Maggid,

Iringa.

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye7kyVsRNjure__BP_cxdWtozimCOkYCJsUTyL38THicZQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments