[wanabidii] WANAOMBAGUA MWANAMUZIKI DIAOMOND WACHUKULIWE HATUA

Friday, September 18, 2015

MWANAMUZIKI DIAMOND NI MWANADAMU TENA MTANZANIA , MWANA AFRIKA MASHARIKI KAMA SISI . MAFANIKIO YAKE NI MAFANIKIO YETU SOTE KAMA JAMII . KAMA MICHAEL JACKSON ALIVYOPATA MAFANIKIO NI USA ILIFAIDI NA INAENDELEA KUFAIDI ( MFALME WA POP ) .

SUALA LA KUANZISHA KAMPENI YA KUMKATAA , KUAMBIA WENZAKO WASIMPIGIE KURA KISA TU AMEONEKANA KWENYE MKUTANO WA KISIASA WA CHAMA USICHOKIKUBALI SIO UZALENDO , SIO UTU NA SIO UMOJA NA AMANI TUNAYOIPIGANIA .

KITU AMBACHO DIAMOND NA WASANII WENGINE WANAFANYA NI BIASHARA AMEUZA BIDHAA YAKE YA KUIMBA NA KUJIINGIZIA KIPATO KWA AJILI YA MAISHA YAKE , FAMILIA NA TAIFA KWA UJUMLA . TUHESHIMU KAZI ZA WATU .

MBONA WEWE NI DAKTARI LAKINI UNATIBU WATU WA IMANI , CHAMA AU RANGI TOFAUTI , JE UNATAKA TUSIJE KWAKO KWA SABABU YA CHAMA AU IMANI YAKO ?

MBONA BABAKO NI MWANAMUZIKI , JE UNATAKA TUSIENDE KWENYE SHOW ZAKE WALA KUNUNUA KAZI ZAKE KWASABABU TU AMEIMBA KIONJO KWENYE NYIMBO ZA HAMASA ZA CHAMA CHAKO ?

MBONA MAMAKO NI MKULIMA JE UNATAKA TUSINUNUE VYAKULA VYAKE KWASABABU AMEVAA FULANA YA CHAMA FULANI ?

TAASISI ZA ULINZI NA USALAMA ZIKAMATE WATU HAWA KWASABABU WANAHARIBU JINA LA MTU , WANADIDIMIZA UZALENDO NA KUJENGA UTENGAMANO KATIKA JAMII AMBAYO SIKU ZOTE UKO MOJA KWA SHIDA NA RAHA .

HALI HII ISIACHWE IENDELEE ITASABABISHA MADHARA KWA JAMII , WATU WATAACHA KUFANYA SHUGULI ZAO NCHINI , UZALISHAJI UTAPUNGUA , UWEKEZAJI UTAPUNGUA NA MASLAHI MAPANA YA NCHI YANAVURUGWA .

YONA FARES MARO
0786 806028


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments