Ndugu zangu siyaandiki haya kwa chuki ila nayaandika haya ili kuwafumbua macho kwa wale wote wanaoishi kwa kutegemea mfuko wa Lowassa na marafiki zake ili waanze kufunguka akili mapema wasije kuumbuka.
Nafahamu kwamba wengi mmekuwa mfukoni kwa mzee Lowasssa kwa muda mrefu sasa takribani miaka mitano mkiangaika kuitimiza ndoto yam zee ya kukalia kiti pale magogoni na wengi mnaamini kuwa bila Lowassa hakuna maisha, fungukeni mtakuja kuaibika
Wengi wenu hamuoni maisha ila mgongoni mwa Lowassa hata alipotoka ccm kwa mbwembwe nyingi mlifuata ili maisha yaendelee kama siku zote na kumpa matumaini kuwa safari bado ipo ili asije asikate tamaa nanyi mkono uende kinywani kama kawaida na watoto waende shule.
Hata hivyo angalizo langi kwenu ni kwamaba maisha ya kisiasa yam zee Lowassa yataishia October 25 ambapo zimebakia ziku chache mno takribani siku 35 tu.
Itakapofika October 25 mwaka huu, ambapo watanzania wenye hki ya kupiga kura watakapotumia haki yao na kikatio chao dhidi ya Lowassa na kumpeleka magufuli Magogoni na hapo ndipo ndipo mwisho wenu na ukawa utakapokuwa umefikia.
Baada ya hukumu hiyo ya kisiasa na ukawa, Lowassa hatabaki mjini tena, bali atahamia kijijini kwake Monduli kuendelea na shughuli zake za ufugaji wa ngombe wake waliosalia bada y wengine kuuzwa kwa ajili urais.
Itakapotokea hilio wengi wenu mtakuwa hmn maisha nje ya Lowassa kwa kwa kuwa safri ya tangu mwaka 1995 itakuwa imeishia hapo, ni muhimu kwa siku hivi takribani 35 zilizobakia mkaanza kujiandaa na misha kijijini kwa Lowassa kumsaidia kuchunga ng'ombe na wengine kuangukia pua kwani mrija utakuwa umeshakata ghafla wengi wenu kuchanganyikiwa mtaumia sana lakini ndiyo maamuzi ya watanzania yatakuwa hivyo.
Naamini , baada ya kutangazwa kwa matokeoya uchaguzi mkuu huo ambapo naamini matokeo kwa asilimia kwa asilimia 100 kwamba dk. Magufuli atashinda kwa aailimia zaidi ya 70 hapo ndipo msamiati wa kushindwa na kusalitiwa itamwingia Lowassa.
Ndipo hapo Lowassa polepole atakapoanza kujitenga na wapambe na kufunga mfuko wake tutashuhudia njaa na vilio kwa wapambe hao, hapo ndipo Lowassa atakapobaini kuwa kumbe hakuwa na mafuriko ila yalikuwa ni mabarafu ambayo yakipigwa na jua humung'uka taratibu na kuishia zake.
0 Comments