[wanabidii] Kwa mama NKYA!!!!!

Saturday, September 19, 2015
Kwako Mama Nkya
 
Salaam!!
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifatilia mwenendo wa mijadala unayochangia katika majukwaa mbalimbali. Wewe ni mmoja wa watu/wanaharakati mliojipambambanua mbele ya jamii kwa muda mrefu na kutuaminisha kuwa ninyi watu wa aina gani.
 
Nimesoma kwa umakini sana makala yako uliyoipa jina "CCM WANAJIDANGANYA", kimsingi ni makala nzuri japo sio bora kama ambavyo nilitegemea kitu bora kutoka kwa mtu wa kariba yako.
 
Napenda kujadili sana mada hiyo ila tafadhali naomba nisaidie majibu ya maswali yangu yafuatayo yanayotokana na mkanganyiko nilioupata kwa maneno yak ohayo.
 
(A) Umesema "…Chama cha Mapinduzi (CCM) na  serikali yake  wanapaswa  wasijidanganye  kwamba kwa kumteua Dr John Magufuli kuwa mgombea  wa Urais  chama hicho kimekuwa kisafi..."
1.      Je, usafi na AU uchafu wa chama unatokana na nini?
2.      Kwa  mtazamo wako CCM si kisafi? Ulitegemea CCM wafanye nini ili kuwa safi katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu?
3.      Je, Unaamini katika "KUJISAHIHISHA"?
 
(B)        Umesema "…Hivyo hakuna mamtiki yoyote kwa CCM kutumia propaganda kwamba  kwa mgombea wake wa Urais  kupata watu kwenye mikutano ya  kampeni basi  tayari kimeshinda kwa asilimia 69.3…… Kama  umati wa watu  ndicho kigezo  cha ushindi  wa  CCM ….".
1.      Bila shaka ni wazi kuwa unatambua kuwa CCM ni taasisi na si kijiwe cha wahuni. Kwa maendeleo endelevu ya Taasisi yoyote ni budi iwe na idara/kitengo maalumu kwa ajili ya M & E. N a kama taasisi bila shaka CCM ina "policy kuhusu namna ya kutathimini mwelekeo wake.
2.      Je ni dhambi kwa taasisi kufanya tathmini na kutoa matokeo kwa umma?
3.      Una ushahidi gani wa kutuaminisha kuwa CCM wametumia kigezo cha wingi wa watu katika kampeni kutoa tathimini yao?
4.      Je  propaganda  ni nini na kwa nini?
5.      Je, unachokifanya ni sehemu ya hizo propaganda au?
 
(C)  Umesema "…Rais  Jakaya Kikwete katika kipindi ccha utawala wake  amesafiri nje ya nchi mara 409  na safari hizo ziligharimu  shilingi  trilioni 4.5……Maana yake angalao kila mwaka Rais alisafiri nje ya nchi mara  40 akipoteza siyo tu fedha alizotumia kwa safari hizo bali pia muda  mwingi wa kuwatumikia Watanzania…."
1.      Katika maelezo yako hayo hapo juu,je unaweza kutuainishia bajeti ya serikali kwa Idara ya Itifaki kwa mwaka kuanzia mwaka 2005 hadi sasa?
2.      Kama hujakurupuka na kumeza matango poli kasha kuwatapikia watanzania kuhusu jambo hilo, Je unaweza kutuaninishia  kutuainishia safari hizo na bajeti yake kwa kila safari ili tujiridhishe na tarakimu uliyotaja hapo?
3.      Unaposema alipoteza muda wa kuwatumikia watanzania kwa hizo safari, Je zilikuwa safari zake binafsi [I mean was it for the personal issues/family matter or for the sake of our country?
4.      Ikiwa unaamini, kama mimi ninvyoamini kuwa zilikuwa safari za kikazi; Je unaweza kuueleza umma wa Tanzania Impact ya kila safari ya Mh.Raisi with reference to matumizi kwa kila safari?
 
(D) Umesema "…Je CCM  na  serikali ya CCM yake  mwaka huu  2015  watatumia kwa 'goli la mkono' kuzuia maamuzi  ambayo wananchi wa Tanzania  watakuwa wamefanya  kupitia sanduku huru la kura kuhusu hatma ya uongozi wa nchi yao …?"
 
1.      Napata shida kuitafakari kauri hii,Je umetumia kigezo gani  kusema " ..watanzania watakuwa wamefanya kupia sanduku huru.." Je tayari una majibu ya jambo ambalo hatujalifanya? Kama hivyo ndivyo ni hatari sana kwa kuwa ni sawa na mtu anayeingia uwanjani akiwa na matokeo mkononi.Nini kitatokea ikiwa atashindwa?
2.      Ikiwa na wengine watakuwa na mawazo kama yako,huoni kama ni hatari kwa kuwa hamtakuwa tayari kupokea matokeo kwa kuwa tu mnaamini kuwa "mtaibiwa kura" na ccm hata kama haitakuwa hivyo?
 
Nitashukuru ikiwa maswali  haya yatapatiwa majibu.


Asante

 
______________________________
Without "Ethical Culture" there is No Salvation for Humanity
______________________________
A D D R E S S
John J. Malata
Tutor. Vikindu TC
P.O  Box 16268
DAR ES SALAAM
TANZANIA 
Mobile:    +255 782366090
Blog:http://pengotz.blogspot.com/

Share this :

Related Posts

0 Comments