[wanabidii] ​JUBILEE NA RUTO, UKAWA NA LOWASSA!

Saturday, September 19, 2015

​JUBILEE NA RUTO, UKAWA NA LOWASSA!

Na Daniel Mbega
JUMANNE ya Agosti 4, 2015 wabunge wa Jubilee nchini Kenya waliamua kwa 'nia moja' kumsafisha na kumtakasa Makamu wa Rais William Kipchirchir Samoei arap Ruto baada ya kuitupilia mbali ripoti ya uchunguzi kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma kuhusiana na ndege aliyotumia kiongozi huyo kutembelea mataifa kadhaa mnamo 2013.
Uchunguzi huo ulikuwa unafanywa dhidi ya kashfa ya ukodishaji wa ndege hiyo maarufu kama "Hustler's Jet" ambapo  mamilioni ya fedha za umma yalitumika.
Uamuzi wa kuitupilia mbali ripoti hiyo ukawaacha midomo wazi wabunge wa upinzani na baadhi ya wanachama wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambayo kwa mujibu wa ratiba ya Bunge, ripoti hiyo ilikuwa miongoni mwa miswada kadhaa ambayo ilipaswa kupigiwa kura baada ya mjadala kuihusu kukamilika Julai 30, 2015.
Lakini kwa mshangao mkubwa, ripoti hiyo ilijadiliwa haraka haraka kabla ya kutupiliwa mbali, licha ya kuwasilishwa bungeni tangu Aprili 2014. Ripoti hiyo ilikuwa ikimlaumu Rais Uhuru Kenyatta kwa kumwagiza Ruto kusafiri katika mataifa manne, mwezi mmoja tu baada ya serikali yake kuingia madarakani.
Mbunge wa Suba John Mbadi, ambaye pia ni mwenyekiti wa ODM alisema kulikuwa na njama za siri kuhusu jinsi ripoti hiyo ilivyojadiliwa. "Haiwezekani ripoti iliyokaa katika Bunge kwa karibu mwaka mmoja kutupiliwa mbali huku mjadala wake ukionekana kutotiliwa maanani. Ni kana kwamba kuna mtu anayelengwa kulindwa na ripoti hii."
Ruto alisafiri katika mataifa ya Congo Brazaville, Ghana, Nigeria na Gabon kati ya Mei 16 na 19, 2013. Uchunguzi wa ripoti hiyo ulionyesha kuwa jumla ya Shilingi za Kenya 18.9 milioni (takriban TShs. 369.6 milioni) zilitumika katika ziara hiyo, wakati ambapo stakabadhi zilionyesha kuwa zilizotumika ni KShs. 100 milioni (TShs. 1.9 bilioni)...
http://www.brotherdanny.com/2015/09/jubilee-na-ruto-ukawa-na-lowassa.html​

--
DANIEL MBEGA
INVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
               www.brotherdanny5.blogspot.com

"Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?" Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, 1995

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments