NANI ANAWAFADHILI CCM, UKAWA?
Na Daniel Mbega
KILIO cha muda mrefu cha Watanzania ni kudumaa kwa maendeleo na kukua kwa tabaka la maskini kunakochangiwa na mfumo usio rasmi wa ufisadi uliotamalaki kiasi cha kuua maadili ya utumishi wa umma.
Misingi imara iliyowekwa na waasisi wa taifa hili imevunjwa kwa makusudi na wale waliopewa dhamana ya uongozi, jambo ambalo limefanya pengo kati ya walionacho na wasionacho liwe kubwa zaidi.
Japokuwa ufisadi umekuwepo kwa miaka mingi nchini, lakini kashfa zimewekwa hadharani katika kipindi hiki cha awamu ya nne ya uongozi wa Jakaya Kikwete, ambaye pamoja na kushindwa kutoa maamuzi magumu katika baadhi ya mambo, lakini amethubutu kuweka uwazi na kuacha sheria ichukue mkondo wake kwa baadhi ya watu waliotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu kuna maswali mengi ya kuwauliza wanasiasa, hususan wa CCM na wale wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwamba fedha wanazofanyia kampeni wamezitoa wapi.
Pamoja na ukweli kwamba ipo Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 na Sheria Namba 1

ya Uchaguzi ya mwaka 1985, lakini kwa hali inavyoonekana sheria hizi hazifuatwi kwani dhahiri gharama zinazotumiwa na vyama hivyo ni kubwa kuliko sheria inavyoelekeza.
Sheria ya Gharama za Uchaguzi inaagiza, gharama za kampeni kwa Mbunge zinapaswa kuwa Shs. 30 milioni na zisizidi Shs. 80 milioni kulingana na ukubwa wa jimbo husika, na kwa upande wa kampeni za urais, zinapaswa zisizidi Shs. 6 bilioni.
Sheria ya Gharama za Uchaguzi madhumuni yake ni kujenga mazingira yatakayowezesha kuwapo kwa uwazi zaidi katika matumizi ya fedha zitakazotengwa kwa ajili ya kampeni, pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa ndani ya vyama vya siasa katika uteuzi wa mgombea na uchaguzi wenyewe kwa ujumla.
Sheria hiyo inaelezea masharti kuhusu fedha zitakazotumika kwa ajili ya uchaguzi, maana ya gharama za uchaguzi, uchaguzi ndani ya Vyama vya Siasa, gharama ambazo vyama vya siasa vinapaswa kutumia wakati wa uchaguzi, masharti kwa Vyama vya Siasa na wagombea kutoa taarifa kuhusu gharama zitakazotumika wakati wa uchaguzi.
Aidha, sheria hiyo inazungumzia kuhusu michango au misaada inayotolewa na kupokewa na vyama vya siasa, kuzuia fedha kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kampeni za uchaguzi, matumizi ya gharama kwa vyama na taasisi za kiserikali wakati wa kutoa elimu ya Kampeni na chaguzi za kisiasa.
Tumeshuhudia jinsi chaguzi za ndani za kura za maoni kwa CCM na Chadema zilivyogubikwa kwa rushwa na kuna baadhi ya wagombea ambao walidakwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wengine wakaenguliwa na vyama vyao kwa matukio hayo.
Sehemu ya tano ya sheria hii inahusu masharti yanayokataza baadhi ya matumizi ya fedha kama gharama za kampeni na uchaguzi. Matumizi hayo ni yale yanayohusu gharama kwa vitendo vinavyozuiwa au kuwa haramu wakati wa kampeni na uchaguzi.
Sheria inasema kila chama cha siasa kitagharamia kampeni za uchaguzi kwa kutumia gharama za uchaguzi zinazotokana na vyanzo vyake, kwa mujibu wa kifungu cha 8(1) cha sheria hii. Na kifungu cha 8(2) kimezingatia kuwa mgombea anaweza kutumia gharama zake mwenyewe wakati wa kampeni pale inapobidi kulingana na mahitaji ya kampeni zake.
Sheria hii inaweka sharti la uwazi katika mapato na matumizi ya vyama na wagombea kwa ajili ya uchaguzi kabla, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi na katika kifungu cha 9(1), inasema: "Mgombea atatakiwa kutoa taarifa ya fedha alizonazo na anazotarajia kupata na anakusudia kuzitumia kama gharama za uchaguzi ndani ya siku saba (7) baada ya siku ya uteuzi. Taarifa hizo zitawasiliskwa kwa Katibu Mkuu wa chama kwa mgombea wa nafasi ya Urais na kwa mgombea wa nafasi ya Ubunge na Udiwani taarifa zake ataziwasilisha kwa Katibu wa Chama wilaya."
Kila chama cha siasa kinachoshiriki katika uchaguzi ni lazima ndani ya siku thelathini (30) baada ya siku ya uteuzi wa wagombea kufanywa na Tume ya Uchaguzi kitoe taarifa kwa Msajili juu ya fedha zote ambazo kinakusudia kutumia kama gharama za uchaguzi; na kutumia kwa kuwadhamini wagombea wa chama hicho zikiwa ni kama gharama za uchaguzi.
Pamoja na maelekezo hayo ya Sheria, lakini bado hakuna atakayekuwa na uhakika zilikotoka fedha hizo, zina masharti gani na ni kiasi gani hasa, kwa sababu naamini hakuna anayeweza kueleza kiwango halisi cha bajeti yake – si kwa...
http://www.brotherdanny.com/2015/09/nani-anawafadhili-ccm-ukawa.html--
DANIEL MBEGA
INVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
www.brotherdanny5.blogspot.comINVESTIGATIVE JOURNALIST, BLOGGER, RESEARCHER & PUBLISHER
CELL: +255 767 939 319/ +255 715 070 109
WHAT'S APP: +255 656 331 974
BLOGS: www.kilimohai.wordpress.com
"Kama hawatuwekei mgombea mzuri, kwanini watutawale?" ~ Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, 1995
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAE93EM_8LrDcb79-%3Dv627TC9-FPmpr%2BOzBLHPXWqCmMD9a9AfQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments