Na JOHNSON MWAMBO
Huwa nashangaa kwamba Lowassa mwenyewe na kina Mbowe, Lissu, Baregu nk wanapozungumzia tuhuma zinazomwandama za ufisadi wanaishia kwenye Richmond tu! Nimemsikia Lowassa akijitetea kwamba alilazimishwa na Rais Kikwete kutia saini mkataba ule wa Richmond!
Sawa, yawezekana alilazimishwa lakini tuhuma zinazomwandama kwamba si mwadilifu hazihusiani na Richmond tu. Ni tuhuma za muda mrefu hata kabla ya Richmond. Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alipomkataa Lowassa kwamba si msafi kimaadili, na hivyo hastahili kufikiriwa urais, kulikuwa na skandali ya Richmond? Skandali ya Richmond si ilitokea wakati Nyerere ameshakufa?
Hata hivi majuzi, mjini Dodoma, kwenye vikao vya CCM vilivyojadili majina ya wawania urais kwa tiketi ya chama hicho; hasa kile cha Kamati ya Maadili na Usalama, hoja iliyotumiwa kuondoa jina lake haikuwa ya Richmond tu. Ilikuwa ni hoja ya jumla kwamba utajiri mkubwa wa huyo bwana unatia shaka kwa sababu haulingani na nyadhifa alizopata kushika serikalini.
Mashabiki wake ndani ya NEC walipochachamaa kumtetea mtu wao Lowassa, ndipo marais wawili wastaafu – Mzee Mwinyi na Ben Mkapa walipozungumza na kuweka wazi kwamba "wanamsitiri" tu vinginevyo wangeweka hadharani mambo mengi yanayomfanya Lowassa aonekane kama mtu asiye mwadilifu; maana walikuwa na faili lake (la Usalama wa Taifa?!).
Na hiyo tunaambiwa ya kwamba ni baada ya Rais Kikwete kuuambia mkutano ule wa NEC kwamba utajiri usio na maelezo ya kuridhisha wa Lowassa umeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 1995 alipokataliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere!
Kwa hiyo, naweza kusema kwa uhakika kabisa ya kwamba marais wanne walioitawala nchi hii – yaani Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa Jakaya Kikwete, wote wamemkataa Lowassa kuwa hafai kuwa rais wa Tanzania kwa sababu ana nakisi kwenye uadilifu!
Katika hali hiyo, mtu unaweza kujiuliza; hivi Chadema walipata wapi ujasiri wa kumsimamisha mtu wa namna hiyo kuwa ndiye mgombea urais wao? Nawaomba wanapojaribu kumsafisha Lowassa, wasiishie tu kwenye Richmond. Waueleze umma ni kwa nini marais wanne (ambao kimsingi ndo hupokea ripoti za mwisho na sahihi kabisa za kiintelijensia) walikataa Lowassa asigombee urais!
Hivi wote hao wanne – Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete walikuwa au wanazo chuki binafsi na Lowassa? Hivi mimi (Mbwambo) ninayeandika haya nina chuki binafsi na Lowassa? Hivi wote wanaoona Lowassa hana sifa za kuwa rais wetu, wana chuki binafsi naye? Naamini jibu ni hapana.
Hakuna mwenye chuki binafsi naye; bali kinachoangaliwa ni maslahi mapana na ya miaka mingi ya nchi yetu. Hakuna atakayehangaika na Lowassa kama atabakia kuwa mwanachama tu wa Chadema na raia wa kawaida anayeendesha biashara na maisha yake binafsi! Tatizo hapa ni yeye kutaka kuwa rais wetu ilhali kwa miaka 20 anaandamwa na tuhuma za ukosefu wa uadilifu,
Chanzo Raia Mwema
-- Huwa nashangaa kwamba Lowassa mwenyewe na kina Mbowe, Lissu, Baregu nk wanapozungumzia tuhuma zinazomwandama za ufisadi wanaishia kwenye Richmond tu! Nimemsikia Lowassa akijitetea kwamba alilazimishwa na Rais Kikwete kutia saini mkataba ule wa Richmond!
Sawa, yawezekana alilazimishwa lakini tuhuma zinazomwandama kwamba si mwadilifu hazihusiani na Richmond tu. Ni tuhuma za muda mrefu hata kabla ya Richmond. Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alipomkataa Lowassa kwamba si msafi kimaadili, na hivyo hastahili kufikiriwa urais, kulikuwa na skandali ya Richmond? Skandali ya Richmond si ilitokea wakati Nyerere ameshakufa?
Hata hivi majuzi, mjini Dodoma, kwenye vikao vya CCM vilivyojadili majina ya wawania urais kwa tiketi ya chama hicho; hasa kile cha Kamati ya Maadili na Usalama, hoja iliyotumiwa kuondoa jina lake haikuwa ya Richmond tu. Ilikuwa ni hoja ya jumla kwamba utajiri mkubwa wa huyo bwana unatia shaka kwa sababu haulingani na nyadhifa alizopata kushika serikalini.
Mashabiki wake ndani ya NEC walipochachamaa kumtetea mtu wao Lowassa, ndipo marais wawili wastaafu – Mzee Mwinyi na Ben Mkapa walipozungumza na kuweka wazi kwamba "wanamsitiri" tu vinginevyo wangeweka hadharani mambo mengi yanayomfanya Lowassa aonekane kama mtu asiye mwadilifu; maana walikuwa na faili lake (la Usalama wa Taifa?!).
Na hiyo tunaambiwa ya kwamba ni baada ya Rais Kikwete kuuambia mkutano ule wa NEC kwamba utajiri usio na maelezo ya kuridhisha wa Lowassa umeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 1995 alipokataliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere!
Kwa hiyo, naweza kusema kwa uhakika kabisa ya kwamba marais wanne walioitawala nchi hii – yaani Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa Jakaya Kikwete, wote wamemkataa Lowassa kuwa hafai kuwa rais wa Tanzania kwa sababu ana nakisi kwenye uadilifu!
Katika hali hiyo, mtu unaweza kujiuliza; hivi Chadema walipata wapi ujasiri wa kumsimamisha mtu wa namna hiyo kuwa ndiye mgombea urais wao? Nawaomba wanapojaribu kumsafisha Lowassa, wasiishie tu kwenye Richmond. Waueleze umma ni kwa nini marais wanne (ambao kimsingi ndo hupokea ripoti za mwisho na sahihi kabisa za kiintelijensia) walikataa Lowassa asigombee urais!
Hivi wote hao wanne – Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete walikuwa au wanazo chuki binafsi na Lowassa? Hivi mimi (Mbwambo) ninayeandika haya nina chuki binafsi na Lowassa? Hivi wote wanaoona Lowassa hana sifa za kuwa rais wetu, wana chuki binafsi naye? Naamini jibu ni hapana.
Hakuna mwenye chuki binafsi naye; bali kinachoangaliwa ni maslahi mapana na ya miaka mingi ya nchi yetu. Hakuna atakayehangaika na Lowassa kama atabakia kuwa mwanachama tu wa Chadema na raia wa kawaida anayeendesha biashara na maisha yake binafsi! Tatizo hapa ni yeye kutaka kuwa rais wetu ilhali kwa miaka 20 anaandamwa na tuhuma za ukosefu wa uadilifu,
Chanzo Raia Mwema
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments