[wanabidii] Kuna haja ya CCM kuendelea kuwa na kura za maoni?

Thursday, August 13, 2015

Mwaka huu tena tumejionea mchakato wa kupata wagombea nafasi za uwakilishi kupitia CCM. Kila wakati kama huu watia nia huunda timu za ushindi. Matumizi ya timu hizi au wapambe hawa kuna madhara makubwa sana baada ya kupatikana mshindi. Mengi hayavunjwi na yamekuwa ndio chanzo cha mpasuko ndani ya chama.
Aidha, kuna kiwango kikubwa cha utoaji rushwa katika michakato hii. Wakati wa mchakato huu nilibahatika kutembelea wilaya tatu na kiukweli nilishangazwa na utoaji wa rushwa unaofanywa na watia nia. Zinatolewa wazi wazi bila kificho. Nilikuwepo wilaya moja mkoani Manyara na nikashuhudia jinsi watu wanavyorudia kupiga kura hata mara tatu. Yote hayo yanafanywa ili kumlinda mtu anayependwa na uongozi wa chama wa wilaya. Nimefurahi kura zinarudiwa katika wilaya hiyo. Natumai chama kitaweza kusimamia vzr hilo zoezi.
Najiuliza maswali mengi ya msingi; je hali hii haijulikani na chama? Je taasisi nyingine hazijui hili? Tutapata viongozi wa namna gani kwa maendeleo ya taifa letu? Kubwa zaidi ni hii ya watanzania kukubali kuuza haki zao kwa vitu vidogo vidogo je tunatarajia maendeleo kweli?
Mwisho naomba CCM itafute njia muafaka ya kuchuja wagombea vinginevyo tutapata viongozi watoa rushwa.
Enyi wapenzi za CCM kina kaka Mpombe na Muhingo na wengineo shaurini chama kitumie njia mbadala
Naomba kuwasilisha

Sent from My Ipad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments