[wanabidii] CCM imeanza kuzaliwa upya na kutakaswa

Monday, August 17, 2015

CCM imeanza kuzaliwa upya na kutakaswa

CCM ni chama kikongwe na chenye nguvu kubwa barani Africa. Ni chama pekee chenye mikakati chanya na yenyetija ukilinanisha na vyama vingine vilivyoleta uhuru Tanzania.

Kwa muda mrefu chama hiki kimepitia katika kipindi kigumu sana na ilikuwa ni vigumu kukitakasa katika kipindi hicho. Kuna kitu Yesu alisema msiyang'oe magugu yaacheni yamee na ngano yakikomaa tutayaona. Kweli sasa hivi magugu yameonekana na lazima yatoke.

CCM sasa imeimarika na inakuwa na nguvu mpya katika uringo wa siasa Africa. Kimeonesha demokrasia iliyokomaa na kuwakumbusha watanzania maadli ndani ya chama ni muhimu sana. Yeyote anayekiuka maadili lazima awajibishwe kwa vitendo. Na pia ni fundisho katika vyama vichanga kama "CDM, CUF NCCR nk" vijifunze kutokana na CCM chama kilichosheheni watu waliosoma Political Science.

Baada ya makando kando kuanzakujiengua yenyewe sasa hivi CCM inaendelea kuwa safi na kuimarika zaidi. Vyama vya siasa Africa havina budi kujifunza kutoka CCM. Ni chama kinachofuata maadili na kusimamia. Heshima kwa Mzee Kinana kwa kukijenga chama na hakika tutazidi kuenzi miaka yote. Pia tunamuheshimu Ash Rose Migiro kwa kusimamia na kujenga chama na wengine wote ambao sijawataja.

CCM imejenga demokrasi kwenye nchi yetu, pomoja na kwamba vyama vya upinzani vimeshindwa kujifunza demokrasia miaka 20+ bado vinavyaa nepi. Viongozi wake wanalia lia tu na sasa wamegeuza vyama vya siasa kuwa biashara. Hii ni hali mbaya sana. Nawasihi vyama vya upinzani kuanzia mwaka 2016 muanze kujengwa vyama vyenu ili ifikapo mwaka 2035 muweze kusimamisha mgombea wenu mliyemjenga na muweze kushinda.

Chama kinapofikiria kusimamisha mgombea uraisi kijue kuwa Urais ni taasisi. Sasa iweje mtu mmoja na hamjawahi kukaa na kumjenga kufuata maadili na miiko ya chama chenu aje moja kwa moja paka chumbani? Lazima vyama vya upinzani vistep down mwaka huu kwenye urais na vijikite kwenye ubunge viweze kujijenga, la sivyo vitapoteza dira na kuchukua mda mrefu tena kujijenga.

CCM sasa hivi imetua mzigo mzito iliokuwa imeubeba, ule mtandao sasa umefutika na CCM imara imezaliwa mara ya pili na imetakaswa. CCM mathubuti aliyokuwa anaisema Mwalimu Nyerere ndio hii sasa. CCM Mathubuti sasa itatufanya kuvuka kwa kasi na kuendelea mbele. CCM mathubuti ndio hii italifanya bara la africa kujifunza.


Huu ni utakaso wa CCM ni utakaso wa Tanzania.
25 Oct 2015 CCM itashinda kwa kishindo
Kumbuka "Umoja ni Ushindi"
  • like

Share this :

Related Posts

0 Comments