[wanabidii] wananchi wa Mwanza wafunga barabara ili kumsalimia Magufuli,

Sunday, July 19, 2015
wananchi w Mwanza wafunga barabara ili kumsalimia Magufuli,

Shughuli za usafirishaji jana zilisimama kwa zaidi ya saa mbili,
baada ya msafara wa mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM),
Dk. John Pombe Magufuli, kupita jijini hapa.

Licha ya kusimama kwa usafiri, msafara huo pia ulizuiwa kwa muda
na wananchi katika eneo la Pasiansi, Kona ya Bwiru na Makongolo,
wakishinikiza kusalimiana na mgombea huyo.

Magufuli ambaye aliongozana na viongozi mbalimbali wa CCM,
serikali, madhehebu ya dini na wananchi wengine kutoka ndani na nje ya
mkoa wa Mwanza alitua Uwanja wa Ndege saa 7:50 mchana.

Baadhi ya viongozi wa CCM taifa waliokuwa wameongozana na Dk.
Magufuli ni pamoja na Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho, Nape
Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania Bara, Rajabu
Luhavi.

Kadhalika, Dk. Magufuli alikuwa amefuatana na mkewe, mama Janet
Magufuli. Msafara wa Magufuli kuelekea ofisi za CCM mkoani hapa
uliondoka uwanja wa ndege Mwanza majira ya saa 8:30.

Akijitambulisha mbele ya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mwanza
waliofurika nje ya ofisi ya CCM mkoani hapa, Dk. Magufuli aliwapongeza
wananchi kwa mapokezi yao makubwa, huku akiwataka Watanzania wote
kuendelea kulinda umoja wao kwa nguvu zao zote.

"Ninawashukuru sana kwa mapokezi yenu makubwa…lakini pia
ninawaomba muulinde umoja wetu na tuendelee kushirikiana bila kujali
itikadi za vyama wala rangi zetu,"Dk. Magufuli.

Aliahidi kuisimamia kwa kikamilifu Ilani ya CCM. Alisema
atahakikisha wafanyabiashara ndogo ndogo hawanyanyaswi.
Awali akimkaribisha, Dk. Magufuli, Nnauye alisema CCM hakitasita
kuwashughulikia wanachama wake ambao hulalamika kwamba mchakato wa
kuwapata mgombea urais kupitia chama hicho ulikiuka taratibu.

"Ninapenda kuwaambia kuwa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani
ya chama uliisha salama na tulimaliza salama ingawa kuna baadhi ya
watu wanalalamika lalamika," alisema.

Alisema wanaCCM hao watashughulikiwa na chama iwapo wataendelea na
malalamiko hayo ambayo alisema hayana ukweli wowote.

"Wakiendelea tutawajibu, hasa wazee wetu." alisema huku akishangiliwa.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk. Magufuli kufika Mwanza tangu
achaguliwe na CCM kupeperusha bendera ya chama hicho kuwania nafasi ya
urais kupitia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka
huu

chanzo nipashe

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments