Watanzania kutoka pale ikulu ya magogoni, atakumbukwa kwa mambo mengi
mazuri hususani kwa watu kutoka mikoani kuanzia tarafani mpaka
wilayani kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi chake chote cha miaka
kumi tangu mwaka 2005 alipoingia madarakani mpaka sasa mwaka huu 2015
anapoondoka madarakani.
Miongoni mwa Sekta amabazo zimfanya rais Kikwete kukumbuka ni sekta ya
ujenzi na miundo mbinu iliyopo chini ya waziri wake John
Magufuriamabaye pia ni mgombea wa uris kwa tiketi ya chama cha
mapinduzi, ambapo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Nne,
Serikaliimepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya
barabara namadaraja nchini. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu
wa jumla ya kilometa17,762 zimekuwa katika hatua mbalimbali za
utekelezaji ambapo barabara zenyeurefu wa jumla ya kilometa 5,568
zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Aidha, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 3,873 zinaendelea
kujengwakwa kiwango cha lami, barabara zenye urefu wa jumla ya
kilometa 4,965 zimefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na
Serikali inatafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami. Vilevile,
upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye jumla ya
kilometa 3,356 unaendelea.
Pia serikali ya rais Jakaya Kikwete itukumbukwa kwa ujenzi ujenzi na
ukarabati wa madaraja, hakuna asiyejua kuwa miaka ya nyuma ilikuwa
ikifika wakati wa masika kuna wilaya mbali mbali zilikuwa zinakosa
mawasiliano na mikoa pmoja na miji mikubwa mpaka hali ya mvua
zinapopungu hali hii ilikuwa inawakera sana wananchi kwa kuwa shughuli
nyingi za maendelo zilikuwa zinasimama.
Serikali ya awamu ya nne ililiona hilo na ikadiliki kulivali njuga kwa
fedha zetu za ndani bila kusubiri wafadhili, katika hili hta kama
wapinzani watapinga lakini wanancjhi wanajua ukweli wa hili n hata
kama utafunga safari uende katika maeneo ambayo yalikuwa na tata
katika madaraja utapa majibu yake.
Tumeshudia jumla ya madaraja makubwa 30 yapo katika hatua mbalimbali
za utekelezaji. Kati ya hayo, madaraja makubwa 12 yamekamilika
kujengwa, ambayo ni Rusumo (Kagera), Umoja (Mtwara), Mwanhuzi
(Simiyu), Kikwete (Kigoma), Nangoo (Mtwara), Ruhekei (Ruvuma), Mbutu
(Tabora), Mwatisi (Morogoro), Ruvu (Pwani), Nanganga (Mtwara),
Maligisu (Mwanza) na daraja la waenda kwa miguula Mabatini (Mwanza).
Aidha, madaraja makubwa 6 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi,
ambayo ni Kigamboni (Dsm), Kilombero (Morogoro), Kavuu (Katavi),
Sibiti (Singida), Ruvu Chini (Pwani) na Lukuledi II (Mtwara). Madaraja
makubwa 12 yako kwenye maandalizi ya kujengwa ambayo ni Momba (mpakani
mwa Rukwa na Mbeya), Mwiti (Mtwara), Simiyu (Mwanza), Wami (Pwani),
Ruhuhu (Ruvuma), Ubungo Interchange (Dar es Salaam), TAZARA Flover
(Dar es Salaam), Selander (Dar es Salaam), Daraja jipya la Wami Chini
(Pwani), Pangani (Tanga), Kirumi (Mara) na daraja la waenda kwa miguu
la Furahisha (Mwanza).
Sambamba na ujenzi wa madaraja makubwa, madaraja madogo madogo zaidi
ya 7,200 yamejengwa na kukamilika. katika kipindi cha mwaka 2005 hadi
2015 Serikali pia imeimarisha Mfuko wa Barabara ambapo mapato ya Mfuko
yameongezeka kutoka Shilingi bilioni 73.08 katika mwaka wa fedha
2005/06 hadi Shilingi bilioni 751.7 katika mwaka wa fedha 2014/15
ikiwa ni ongezeko la asilimia 928.6. ni ajabu sana pale kina Mbowe,
Lipumba pamoja na Mbatia wanavyojifanya vipofu katika mafaniko haya ya
awamu ya nne ambayo tangu uhuru yalikuwa kero kubwa kwa wananchi.
wakati Serikali ya Awamu ya Nne inaingia madarakani mwaka 2005,
vivuko vya Serikali vilivyokuwa vinatoa huduma vilikuwa kumi na tano
(15) tu. Hadi kufikia Aprili, 2015, idadi ya vivuko vya Serikali
vinavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini imeongezeka na
kufikia ishirini na nane (28).
kwa upande wa nyumba na majengo ya Serikali, Wizara ya Ujenzi kupitia
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ilijenga nyumba 173 za makazi ya
Viongozi wa Umma na kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba 10,000 za
Watumishi wa Umma ambapo nyumba 643 zilikamilika katika kipindi cha
mwaka 2005 hadi 2015 na nyumba 270 zinaendelea kujengwa.
Aidha,Serikali kupitia TBA imeendelea kuhakikisha kwamba ujenzi wa
nyumba na majengo yanayotumiwa na umma unazingatia mahitaji maalum
hususan kwa watu wenye ulemavu. Suala hili limeendelea kutekelezwa
kupitia miradi ya ujenzi wa majengo yote ya Serikali ambayo Wakala wa
Majengo umesanifu na kusimamia kama ifuatavyo: Jengo la Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa Manyara, Majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya za Bariadi,
Rorya, Kilolo, Nyamagana na Mvomero. Mengine ni jengo la Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi – Kitengo cha Wakimbizi,
Jengo la hospitali ya Manyara na ukumbi wa mikutano na Vituo vya Afya
ya Msingi (Primary Health Centre Institutions – PHCI) – Iringa,
majengo ya Ofisi za Wakuu 6 wa Mikoa ya Katavi, Njombe, Geita na
Simiyu pamoja na majengo ya Ofisi za Wakuu wa Wilaya 19 za Buhigwe,
Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi, Itilima, Kalambo, Kaliua,
Kakonko, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama, Mlele, Momba Nyang`hwale, Nyasa,
Uvinza na Wanging'ombe.
Katika mwaka wa fedha 2014/15, wakati ambao serikali ya awamu ya
imeendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayosimamiwa na
Wizara ya ujenzi inaendelea vizuri.
Kwa upande wa barabara kuu, jumla ya kilometa 504.4 kati ya kilometa
539zilizopangwa kujengwa kwa kiwango cha lami zilikuwa zimekamilika
hadi kufikia Aprili, 2015. Na kilometa 87.75 zilikua zimekarabatiwa
kwa kiwango cha lami. Kwa upande wa barabara za mikoa, kilometa 40.5
zilijengwa kwa kiwango cha lami. Vile vile, kilometa 450 zilifanyiwa
ukarabati kwa kiwango cha changarawe katika kipindi hicho.
Wakati ris Jakaya akiwa anasubiri muda wake ufike akapumzike
hataliacha hivi suala la msongamano mkubwa wa magari katika Jiji la
Dar es salaam, serikali yake kupitia Wizara ya ujenzi na Mamlaka
mbalimbali zikiwemo Halmashauri za Jiji zimechukuliwa hatua mbalimbli
za kukabiliana na tatizo hilo la msongamano wa magari.
Tayari maandalizi ya ujenzi barabara ya njia sita ya Dar es Salaam –
Chalinze – Morogoro (km 200) sehemu ya Dar es Salaam –Chalinze (km
100) imepangwa kujengwa kwa kiwango cha "Expressway".
Maandalizi ya mradi huu utakaotekelezwa kwa utaratibu wa ubia baina ya
Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership - PPP)
yamekamilika na yameanza kufanyiwa.
Aprili, 2015, Mshauri Mwelekezi (Transaction Advisor) ambaye ni
Kampuni ya Cheil Engineering Company Limited kutoka Korea ya Kusini
alikwishateuliwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.72 na amekamilisha
utafiti wa mwelekeo wabarabara (route survey).
Mwelekeo wa barabara uliochaguliwa unaanzia Charambe katika barabara
ya Kilwa kupitia Kisarawe, Kibamba, Kibaha, Mlandizi hadi Chalinze.
Barabara itakuwa na urefu wa kilometa 128 itakuwa ya njia sita (6) na
barabara za juu (interchanges) tano (5) katika maeneo ya Charambe,
Kisarawe, Kibamba, Mlandizi na Chalinze. Pia itakuwa na vituo vikuu
viwili (2) vya kulipia tozo ya barabara (Toll Plaza) maeneo ya
Charambe na Chalinze.
Pia barabara hii itakuwa na eneo la kupumzika (rest station) pale
Visiga na maeneo mawili (2) ya kuegesha malori ambayo yatakuwa Mbezi
na Mbala. Vilevile Mshauri Mwelekezi atafanya utafiti wa jinsi ya
kuunganisha barabara hii kutoka Charambe hadi bandari ya Dar es
Salaam. Kwa sasa Mshauri Mwelekezia naendelea na kazi ya kuandaa
nyaraka za zabuni na baadaye atasimamia taratibu za kumpata
Mbia/Mwekezaji (Concessionaire) wa mradi huu. Gharama za mradi huu wa
ujenzi zinakadiriwa kufikia Shilingi Trilioni 2.397 na utatekelezwa
kwa njia ya Ubia na Sekta Binafsi (PPP).
Tunajua pia kuwa huwezi kuondoa Msongamano wa magari ya jiji Dar ers
Salaam bila kulitaka Daraja la Selander, Rais Jakaya Kikwete
anaondoka magogoni akiwa keshalipati ufumbuzi wa kudumu eneo hilo la
selander, Serikali ya Korea Kusini imekubali kuipatia Serikali ya
Tanzania mkopo wamasharti nafuu kwa ajili ya ujenzi wa Daraja jipya la
Selander. Upembuzi yakinifu wa mradi huu umekamilika na maandalizi ya
kutiliana saini makubaliano ya mkopo wa kugharamia ujenzi wa daraja
kati ya Korea Exim Bank (kwa niaba yaSerikali ya Korea Kusini) na
Serikali ya Tanzania yanaendelea.
Daraja hili pamoja na barabara zake za maingilio litakuwa na urefu wa
jumla ya kilometa 7.2 na litaanzia eneo la Koko Beach kupitia Kenyatta
Drive na kuingia baharini na kisha kuungana na barabara ya Barack
Obama eneo la Hospitali ya Aghakan. Mradi huu tagharimu Shilingi
Bilioni 197.5. Aidha, Daraja la Kigamboni linaendelea kujengwa kwa
gharama ya Shilingi Bilioni 236.524.
Ujenzi wa barabara za juu (flyovers na interchanges) na maboresho ya
makutano ya barabara katika jiji la Dares Salaam,mpkaAprili, 2015 hali
utekelezaji upo kama ifuatavyo kama ifuatavyo: Barabara ya Juu
(Flyover) ya TAZARA: Usanifu wa kina umekamilika chini ya ufadhili wa
Serikali ya Japan. Taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi
atakayekidhi vigezo zinaendelea huko Japan.
Kazi ya ujenzi wa Flyover ya TAZARA ambayo itagharamiwa na Serikali ya
Japan ikishirikiana na Serikali ya Tanzania inatarajiwa kuanza katika
ya mwaka, 2015. Gharama za mradi huu ni Shilingi Bilioni 93.622.
Interchange ya Ubungo Benki ya Dunia imekubali kugharamia utekelezaji
wa mradi wa ujenzi wa barabara za juu (Interchange) katika makutano ya
Ubungo. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Interchange ya Ubungo
umekamilika. Zabuni ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya usimamizi
wa ujenzi zimetangazwa. Serikali inakamilisha taratibu kwa ajili ya
kutangaza zabuni za kumtafuta Mkandarasi wa ujenzi.
Vile vile Interchange ya Ubungo itakuwa na levels tatu ambapo magari
yanayotoka katikati ya jiji la Dar es Salaam kuelekea Morogoro
yatapita chini, magari yanayotoka TAZARA kuelekea Mwenge yatapita juu
na magari yanayokata kulia yatapita katikati. Gharama za mradi huu
zinakadiriwa kuwa Shilingi Bilioni 126.661. Upanuzi wa barabara ya
Gerezani (Bendera Tatu – KAMATA) unakadiriwa kugharimu Shilingi
Bilioni 29.135. serikali inaendelea na maandalizi ya Maboresho ya
Makutano ya Chang'ombe, Magomeni, Mwenge, Tabata, KAMATA, Uhasibu na
Morocco yanaendelea.
Serikali ya Kikwete imeendelea kutekeleza miradi ya barabara za
kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam zenye
urefu wa kilometa 109.35. Barabara hizo ni pamoja na Ubungo Bus
Terminal – Mabibo – Kigogo Roundabout (km 6.4); Kigogo Roundabout –
Bonde la Msimbazi – Twiga/Msimbazi Jct (km 2.7); Jet Corner – Vituka –
Devis Corner (km 10.30); Tabata Dampo – Kigogo (km 1.60); Ubungo
Maziwa – External (km 0.65); Mbezi (Morogoro Road) – Malambamawili –
Kinyerezi –Banana (km 14); Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi
Mwisho (km 20); Tangi Bovu – Goba (km 9); Kimara Baruti–Msewe (km
2.6); Kimara –Kilungule – External Mandela Road (km 9); na Kibamba –
Kisopwa (km 12.0). Pia ukarabati unaoendelea katika barabara za Ukonga
– Mombasa –Msongola , Kimbiji – Tundwisongani, Misheni – Kijichi –
Zakhem, barabara ya Uhuru, Kutengeneza Mifereji ya Maji, uhamishaji
miundombinu maeneo ya miradi, malipo ya fidia, n.k. vyote vinakadiriwa
kugharimu Shilingi Bilioni 181.795.
Pia Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus
Rapid Transit Infrastructure – BRT) ambao unajumuisha Ujenzi wa
Barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kivukoni, barabara ya Kawawa
kutoka Magomeni hadi Morocco na barabara ya Msimbazi kutoka Fire hadi
Kariakoo zenye jumla ya urefu wa kilometa 20.9.
Pia kuna vituo vya mabasi 29, vituo vikubwa vitatu namadaraja ya
waenda kwa miguu matatu. Pia Ujenzi wa Karakana (Depot) na Kituo cha
Mabasi cha Ubungo; Ujenzi wa Karakana (Depot) ya Jangwani; Ujenzi wa
Kituo Kikuu cha Mabasi (Terminal) cha Kivukoni; vyote hivyo mchakato
wake unaendelea kwa hatua mbali mbali, kwa m,tu ambaye anayeishi
mikoani akija nleo Dar es Salaam maeneo ya katikati ya mji atashangaa
kasi ya ejenzi inavyoendelea leo.
Pamoja na juhudi kubwa hizo za serikali ya awamu ya nne lakini bado
wapinzani wamekuwa wakibeza kuwa miradi mingi haitekwelezi napenda
kuwapa changamoto moja wawe wakweli kutoka mioyoni mwao waangali hali
ya barabara zetu leo ni sawa na miaka kumi iliyopita
Bado hatujasahu ndugu zetu walivyokuwa wakiliwa na simba njia ya
kusini ambapo leo unapamba basi kwenda mtwara kutoka dar es Salaam
kwenda mtwara unafika safari yako ndani ya masaa tisa, pia tunakumbuka
wakazi wa kanda ya ziwa walivyokuwa wakiteseka kulala njiani mpaka kwa
siku tatu wakati leo wanafika ndani ya siku moja.
Hatujasahau ndugu zetu wa Kagera walikuwa wanalazimika kutumia mpaka
siku tano kupitia Kenya na Uganda kufika mkoani, kwao hali ni tofauti
na sasa ile hali ya kushuka mipakani na kugonga visa hakuna tena na
gharama za usafiri na matumizi za kupitia Kenya na Uganda hazipo tena.
Haya yaliwezekanaje ndani miaka 10 ya jakaya kikwete na yashindikane
hayo mengine, rais Jakaya anamuachia vema rais ajaye kwenye sekta ya
miundo mbinu, ambayo ni miongoni mwa kero kubwa tangu uhuru kwa
watanzania.
Kwa wale wanaosema rais Jakaya Kikwete hana lolote alilowafanyia
watanzania ningependa kuwaasa jambo moja kuwa wanachofanya ni
kujidanganya kwani watanzania wanajua mengi na yanaonekana kwa macho.
Vile vile niwaambie wabunge wa upinzani walikuwa wakibeza miradi ya
wizara ya ujenzi ya miundo mbinu kuwa miradi hiyo niliyoitaja hapo juu
kuwa haitekelezeki napenda kuwaambia hata huu mtandao wa barabara
nchini walikuwa wakiubeza lakini leo wapo kimya hawana la kusema. Kwa
wale wanaopinga ningewashauri wafunge safari siku moja ya kuzunguuka
nchi yetu kwa njia ya barabara watajionea wenyewe, kwanza wangeanza
safari Arusha kwenda Singida kupitia Manyara.
Halafu angewauliza wanaotoka Dodoma kwenda Iringa kupitia mtera,
halafu nenda njia ya Manyoni hadi kigoma kupitia Tabora, na kwa wakazi
wa kusini akawaulize wanaotoka Masasi kwenda Songea kupitia Tunduru.
Pia aangalie safari ya kutoka Songea kwenda mpaka Sumbawaga.
Kwa wakazi wa kanda ya ziwa angalie Safari ya kutoka Manyoni kwenda
Mwanza kupitia Singida mjini, Nzega, Shinyanga mpaka Mwanza yenyewe.
Halafua anzia Shinyanga kwenda Bukoba. Rudi tena anzia Dar es Salaam
kwenda Lindi na Mtwara.
Nani asiyejua kuwa miaka kumi iliyopita kwa makazi wa Dar es Salam
mwenye asili ya ya mikoa ya Lindi, Mtwara, Kigoma,Rukwa, Simiyu,
Geita, Ruvuma na Katazi wakipata misiba kufika kwao ilikuwa shughuli
pevu kufika makwao.
Mwisho napenda kumpongeza mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe wakati
akichangia hotuba ya wizara ya fedha 2014/2015 kwa mara ya kwanza
nimemshuhudia akiuunga mkono bajeti kwa kusema wakati anaingia
madarakani miaka 4, iliyopita katika jimbo lake kulikuwa na vijiji
vitatu tu vyenye umeme katika vijiji 60 kwa sasa jimbo Ludewa ina
vijiji 50 vyenye umeme na vingine vitapata umeme kabla ya rais
Kikwete kuondoka madarakani, filikunjombe anasema wakati anaingia
madarakani kulikuwa hakuna lami lakini kwa sasa kuna kilometer 50 za
lami kati ya kilometer `200 za barabara katika jimbo lote la Ludewa
na zinaendea kujengwa.
Filikunjombe amesema kuwa kama atapinga mfanikio ya awamu ya nne basi
hata wananchi wake watamkataa, alifika mbali zaidi mpaka kutaja idadi
ya madaraja tata ambayo yalikuwa yanawasumbua kipindi cha masika
lakini kwa sasa yanapitika msimu wote.
Napenda kumalizia kwa kumtakia mapumziko mema na afya tele kwa rais
waetu Jakaya pale muda wake wa kustaafu utakapofika.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments