Nikafikiri kuwa Siasa maana yake ni kuziba masikio na kufungua mdomo? tangu Kingunge alipojitokeza kwa mara ya kwanza kuwa mpambe wa Mtangaza nia, bila kujali yuko nyuma ya nani watu tulimkosoa sana. Maneno yote yaliyosemwa juu ya mwenendo wake huo bado hajasikia? Ameziba masikio? Anapanua mdomomkusema? Hana mshauri? Eti anatishia kuihama CCM? Kuna watu wangapi wa kumfuata Kingunge? au anasubiri 'Mzee' akiamua naye afuate? Hivi anayoyasema kama Lowasa angepitishwa kwenye bora tano angeweza kuyasema? Hivi bado haoni sababu za mchakato kuwa kama ulivyokuwa ili kukinusuru chama? Kama angekuwepo wakati wa Pilato angelifungulia jambazi la Baraba kwa kisingizio kuwa watu wengi wamemtaka? Ninamshangaa kwa kuwalaumu 'wazee'. Akina Mkapa, Karume, Mwinyi. Anasahau kuwa alistahili kuwa mmoja wao. Alistahili kuwa nao akikisaidia Chama alichokianzisha kiendelee kuheshimika kikiwa madarakani au nje ya madaraka (maana lazima siku moja kitatoka madarakani'. Kingunge
hana mshauri? Anamshauri nini?
Nimemaliza mada. Ngoja niseme mambo mengine yasiyohusiana na mada hiyo hapo juu.
1) Uzee mara nyingi huonekana kwenye makunyanzi ya ngozi, na kutembea na mkongojo. Hauonekani kwenye fikra. Ndiyo maana watu wanaoshika mikongojo huendewa na kutakiwa kutoa mawazo yenye busara
2) Siku moja Tembo alikuwa anavuka daraja. Kwa jinsi daraja lilivyokuwa na uzito wa tembo likawa (daraja) linatingishika. Baada ya tembo kuvuka akasikia nzi anasema 'kidogo tulivunje daraja'. Kumbe alikuwa mgongoni mwa Tembo wakati 'wakivuka' daraja.
Nakipongeza Chama Cha mapinduzi kwa kulivuka daraja la kwanza. Kumtafuta mgombea. Haikuwa kazi ndogo
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments