Awali ya yote nikupe pole nyingi kwa kuondokewa na baba mzazi. Mungu ailaze pema kwenye uzima wa milele roho ya marehemu.
Nakuandikia maneno haya machache baada ya kusoma makala yako yenye kichwa cha habari:Kama akiwa Rais Nani atamfunga 'gavana' Magufuli? ambayo nimeipata kupitia
: http://www.raiamwema.co.tz/kama-akiwa-rais-nani-atamfunga-%E2%80%98gavana%E2%80%99-magufuli
Nakupongeza sana kwa kuonyesha mfano wa aina ya uchambuzi ambao wanahabari wanapaswa kufanya ili vyombo vya habari viweze kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya nchi kupata uongozi madhubuti tuendako.
Binafsi ninaamini kuwa ni hadi hapo chama kinachotawala nchi yetu sasa --CCM kitakapoamua kwa hiari au kulazimishwa kuukubali mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa dhati kabisa na kushiriki na wananchi kuweka Katiba Mpya ya kuuendesha mfumo huo ndipo chaguzi zitakapoanza kutoa uongozi wa nchi unaoweza kutoa mchango mkubwa wa kuiondoa nchi katika lindi la umaskini na kudumisha amani ya kweli mioyoni mwawananchi siyo hii amani feki inayozungumzwa majukwaani na wasaka maslahi ya kushika dola ili kujinufaisha mmoja mmoja na kama kikundi kidogo cha watawala.
Uchaguzi nchini kwetu kwa sasa, kwa mtazamo wangu, ni mradi (project) wa kukamata dola basi iwe ni kwa kutumia ufisadi kama ule wa EPA uchaguzi wa 2005 na sasa usanii wa 'usafi' wa mtu mmoja 'bulldozer'(tingatinga) kama ulivyoeleza kwenye makala yako ili mradi kufanikisha kukamata dola wakati nchi nzima inanuka ufisadi ulioasisiwa watawala na chama chao ili kulinda madaraka yao na maslahi yao na wala siyo maslahi ya nchi na wananchi.
Kuendesha mfumo wa vyama vingi kifeki feki, nchi inabamizwa kweli kweli. Ni maumivu makubwa kwa wananchi! Tafadhali anayetaka kujibu nilichoandika hapa aisome kwanza makala ya Mbwambo.
Asante sana Johnson Mbwambo kwa utumishi wa nchi uliotukuka. Mungu akulinde na kukubariki sana kwa mapenzi yako makubwa kwa nchi yetu. Nchi yetu kwanza maana kila mmoja wetu atapita, nchi itabaki, lakini itabakiikiwa katika hali gani kama hatuipendi kwa dhati? Itabaki vipi kama sisi wanahabari hatuna ujasiri wa kuandika ukweli hata kama ni mchungu ili wanaoutaka uongozi wa nchi wajifunze, wakiri makosa, waombe radhi, wabadilike –watoe uongozi mahiri?
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1437827592.4701.YahooMailBasic%40web121003.mail.ne1.yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments