[wanabidii] MBWA DOMO BAYA LAWAMANI KWA KUMTOROSHA BUNDI WA KAMANDA

Tuesday, June 09, 2015








MBWA DOMO BAYA LAWAMANI KWA KUMTOROSHA BUNDI WA KAMANDA RAS MAKUNJA

KOLOKOLONI DOG DOMOBAYA  AMCHEZEA RAFU KAMANDA FFU-Ughaibuni



Jumamosi ya 6 Juni 2015 inasemekana haikuwa nzuri katika kambi ya FFU -ughaibuni  baada ya msimu wa joto kuanza nchini ujerumani ,kikosi maalumu cha kuangalia wanyama kiliungana na Kamanda ras Makunja kumsaka Bundi wa  mkuu
huyo wa Ngoma Africa Band,Bundi maarufu kwa jina la udi udi alichomoka katika
banda maalumu katika makao ya Ras Makunja marufu kama himaya ya Anunnaki Alien, Kutoroka kwa Bundi huyo kumesababishwa na mbwa wa kamanda aitwae Kopro Dogi Domobaya, mbwa huyo anashutumiwa kwa kuwa mzembe na kuupiga kikumbo mlango wa banda la Bundi na kumfanya bundi kutoroka ,kamanda Ras Makunja aliwambia kikosi cha kuangalia wanyama kuwa "huyu mbwa si mlinzi
mzuri siku hizi amekuwa na utoto sana ! mbwa huyu tangu ampewe zawadi ya mpira watoto wa jirani yeye kazi yake ni kucheza na mpira mpaka kavunja banda la Bundi" Ras Makunja akilalamika na kudai kuwa huyu mbwa akiendelea  na uzembe nitamfuta kazi,Pia inasemekana midudu hiyo imetengewa eneo maalumu katika himaya ya FFU-ughaibuni, Bundi huyo baadaye alirudi mwenyewe baada ya kutoweka kwa masaa kadha.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments