Anasema Anamshukuru Ndugu Benjamin Mkapa kwa kuona iko haja ya kuwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa ambayo ni ya Mwaka 2000 mpaka 2015
2018 Wanatakiwa kuwa wametangaza barabara zote za kuunganisha kila mkoa
Miaka mitano ijayo kinachopangwa ni kujenga uwezo wetu kiuchumu kwa kujenga viwanda ambavyo vitalenga kutumia rasilimali za Wakulima na wafugaji wakutoka nchini kwetu
Utawala bora na uhifadhi wa Mazingira lazima waende navyo sambamba
swali: Una kitu gani kipya ambacho unatuletea?
JIBU: Kumuweka mtu ambaye hajui kitu ni kosa, kwani atatumia muda mwingi kujifunza, yeye anayajua yote, Mafanikio yote ya Wizara Kiranja wao ni PINDA. Amefukuza Wakurugenzi na watendaji zaidi ya 2000 Kimyakimya. Sema Waziri wako mkuu sina makeke na Majigambo, na ningekuwa na Majigambo kama wengine mbona mngekoma? Kitu kikubwa ni kuongeza ukuaji wa uchumi wa pamoja, uguse makundi yote. Kusiwe kuna umbali kati ya mwenye nacho na asiye nacho lakini wote wakue kiuchumi
SWALI: Ulisema kwamba ukimaliza muda wako unarudi nyumbani kupumzika na kufuga nyuki, imekuwaje tena umerudi kuutafuta urais?
JIBU: Kwanza nirekebishe kidogo, kauli ile ilikuwa imelenga kwenye jimbo langu kuwa nikimaliza muda wangu, sitarud tena kwenye kugombea Ubunge, lakini ilikuwa 2012. Hata hivyo toka 2012 mpaka sasa nina haki ya kubadili msimamo wangu. Kwa hiyo ndio maana nikaamua kurudi tena. Vievile mkumbuke kuna muda watu huacha wake zao na baadaye humrudia tena.
SWALI: Kuna muda ulikataa kutumia magari ya kifahari imekuwaje mpaka sasa unatumia magari ya kifahari?
JIBU: Magari ambayo niliyakataa ni VX8 ambayo thamani yake ni milioni 300 ambapo kwa fedha hii unapata magari matatu, na nilikataa kwa kuzingatia umuhimu wa mtu na uhitaji wake. Ndio maana mpaka sasa mtu haendeshi gari lolote bila kuniuliza. Nilichohitaji ni kuwa na magari yasiyozidi CC3000. Ndio maana kwenye Halmashauri kwa sasa kuna Toyota Hard top badala ya VX8 na tunaendelea kupunguza kwenye maeneo mengine. Lakini ukiyaangalia mengine tunayotumia ni tofauti na hayo ya milioni 300 japo yana muonekano sawa.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments