ametangaza nia ya kuchukua fomu ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa
ajili ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
Uchaguzi Mkuu ujao.
Balozi Karume alitangaza nia yake wiki iliyopita katika Ofisi ya
Halmashauri ya Wilaya ya Kati Unguja na kuahidi kuwa iwapo chama chake
kitampitisha na kupata ridhaa ya kuingia Ikulu, atatoa uhuru wa
kujieleza kwa wananchi wake na uhuru wa kuikosoa Serikali bila ya
kuvunja sheria na katiba ya nchi.
Alitumia muda mwingi kuelezea historia na uzoefu wake wa uongozi ndani
ya chama na Serikali na kuwataka Watanzania kutokurupuka kumchagua
rais kama watataka maendeleo endelevu.
Balozi Karume alisema ameamua kugombea nafasi hiyo ya urais, baada ya
kujipima na kuona ana sifa na uwezo wa kuliongoza Taifa la Tanzania na
akawakumbusha wagombea wenzake umuhimu wa kuwa na kiongozi atakayeweza
kujenga umoja na kudumisha amani miongoni mwa Watanzania.
"Ni wakati wa kufikiria na kutukuza utaifa wetu, badala ya Utanganyika
na Uzanzibari," alisema Balozi Karume katika mkutano wake huo
uliochukua takriban saa moja na nusu.
Kwa mujibu wa Balozi Karume, urais unahitaji kiongozi mwenye sifa na
uadilifu atakayepiga vita vitendo vya ubadhirifu na kukemea rushwa ili
kujenga Taifa lenye kufuata misingi ya sheria na utawala bora.
"Uongozi si suala la majaribio, hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuwa
makini na watu ambao walishawahi kupewa uongozi na kushindwa kutokana
na kukosa uadilifu," alisema Balozi Karume.
Hata hivyo, alisema kwamba atahakikisha anaendeleza mipango yote ya
maendeleo iliyoanzishwa na Rais Jakaya Kikwete na kukabiliana na kero
mbalimbali zinazowakabili Watanzania hasa suala la umaskini, maradhi
na elimu.
Vipaumbele vyake
Akizungumza katika shamrashamra za kutangaza nia hiyo, Balozi Karume
alisema lengo lake ni kuwania nafasi hiyo ya juu serikalini ili
kupokezana kijiti na kuendeleza mambo yote mazuri yaliyoanzishwa na
mtangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete.
Balozi Karume alitaja kipaumbele chake cha kwanza kuwa ni uhuru wa
watu wote. "Kila mtu ana haki ya kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo
yake kuwa muumini wa dini au chama chochote cha siasa tena bila
kubughudhiwa na mtu mwingine.
"Mkombozi wa mwananchi ni kuimarisha kilimo kwanza, elimu baadaye,
huwezi kusoma huku ukiwa na njaa na hilo ndilo lengo nikipata ridhaa
ya kuwa Rais wa Muungano" alisema Balozi Karume.
Alisema Tanzania ili iweze kujenga uchumi imara, inahitaji kiongozi
mwenye mbinu na uwezo wa kupambana na rushwa na ufisadi kwa vile ndiyo
adui wakubwa wa maendeleo yake.
Alisema kuwa atahakikisha Watanzania wanapata uhuru wa kuchagua chama
wanachotaka, uhuru wa kuabudu dini wanayotaka na kufanya biashara
katika mazingira bora pamoja na kufungua milango ya uwekezaji yenye
masilahi kwa Serikali na wananchi wake.
Alisema uhuru atakaousimamia pia utahusu uhuru wa kujituma na kufanya
biashara bila kuwekewa vikwazo, kwani nayo ni haki ya msingi ya
wananchi wa Tanzania.
"Uhuru wa kujituma ni muhimu sana kwa kila mtu siyo mtu anataka kuuza
njugu wewe unamwambia huna leseni… leseni kwani anataka kuendesha
gari? Mtu akitaka kuendesha gari ndiyo mdai leseni, lakini siyo kuuza
njugu lazima watu wapewe uhuru wa kujituma," alisema Balozi Karume.
Balozi alieleza kuwa atasimamia uhuru wa kuepukana na njaa kwa
kusimamia uanzishwaji wa viwanda ili kusindika mazao na bidhaa
mbalimbali kwa ajili ya kuziongezea thamani.
Karume alitumia muda mwingi kuelezea historia ya nchi na CCM akieleza
kuwa ni muhimu kwa wanachama hao kuwachagua viongozi wenye uelewa
mzuri wa kimataifa na siyo watu ambao wanasindikiza na kutia aibu
mbele ya mabalozi wa nchi za nje.
"Hatutaki mtu wa okay, sir au yes sir! Tunataka mgombea urais ambaye
anaelewa mambo ya kidiplomasia na anajua kuzungumza na mataifa
mbalimbali siyo anakwenda Ulaya anashindwa kuongea badala yake
anaitikia tu yes sir," alisema.
Balozi Karume amewataka wanachama wa CCM kuwachagua viongozi kwa
vigezo vya uwezo na uadilifu na siyo kwa sababu wamekaa muda fulani
katika matawi na mashina ya chama hicho tawala, huku akielezea jinsi
gani wao walivyopikwa katika chama hicho.
Aidha, aliwapiga vijembe wenzake waliotangulia akisema wapo baadhi ya
wagombea ambao wametangaza anataka kuunda Tanzania mpya jambo ambalo
alisema haliwezekani kwani Tanzania ni hiyohiyo na haiwezi kuwa
nyingine.
Alisema watu waliosema hawatakubali kilimo kwanza na badala yake
watawekeza kwenye elimu wamekosea, kwani ingawa elimu ni muhimu,
kilimo nacho bado ni muhimu pia.
Ilivyokuwa ukumbini
Balozi Karume aliwasili katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kati
mkoani Unguja saa 9:45 jioni akiwa ameambatana na Zainabu Shamori
ambaye amewahi kuwa Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Pemba na Kusini
Unguja.
Pia, Zainabu amewahi kuwa Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar wakati wa
uongozi wa Rais Amani Abeid Karume na aliwahi kuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).
Baada ya Balozi Karume kuwasili katika ukumbi huo alipokewa na wapambe
wake ambao ni wanachama wa CCM na baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa
wakiimba na kushangilia kwa kupiga makofi muda wote.
Balozi huyo alipopanda jukwaani, kundi la watu waliokuwapo ukumbini
ambao idadi yao haikufika 100, waliendelea kuimba na kushangilia kwa
kupiga makofi. Hata hivyo, hapakuwapo na shamrashamra za ngoma.
Licha ya uchache wao, watu hao walionekana wenye furaha na
kumshangilia Balozi Karume kwa kila neno alilokuwa akisema hasa pale
alipoelezea namna atakavyopambana kuondoka rushwa na ufisadi
unaoitafuta Serikali na kudhoofisha uchumi.
Huku akiendelea kushangiliwa, Balozi Karume alisema kwamba Rais
mstaafu Karume, ambaye ni kaka yake, alisema kuwa katika Uchaguzi Mkuu
mwaka huu ni vizuri apatikane rais mwenye uzoefu wa kimataifa.
"Rais alisema ni vizuri apatikane rais ambaye atakuwa ametembea nchi
mbalimbali ili ajue uzoefu wa mataifa mengine yanayofanya kazi,"
alisema Balozi Karume.
Balozi huyo aliongeza kuwa uzoefu wa kimataifa ni sifa muhimu kutokana
na kasi ya maendeleo ya kiuchumi inayoendelea duniani hivi sasa.
Katika mkutano huo wa Balozi Karume, hakuna viongozi maarufu waliopo
madarakani au wastaafu waliomsindikiza kama ambavyo imekuwa kwa baadhi
ya wanasiasa wanaotangaza nia ya kuwania nafasi ya kuteuliwa na vyama
vyao kugombea urais.
Siyo mara ya kwanza
Balozi Karume aliwahi kugombea urais wa Zanzibar mwaka 2000, lakini
alijitoa katika hatua za awali na kumwachia Rais Karume, pia mwaka
2005 na mwaka 2010, aligombea urais wa Tanzania Bara.
Wakati akiondoka ukumbini baada ya kutangaza nia jana, Balozi Karume
alitumia muda mwingi kusalimia wanachama waliokuwapo ukumbini kwa
kuwapa mikono.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments