[wanabidii] A New Book By Hamisi Kigwangalla: Kigwanomics and The Tanzania We Want: From Renaissance to Transformation

Saturday, April 18, 2015
Ndugu,

Ninafuraha isiyokadirika kwa hatimaye kufanikisha kazi niliyoianza takriban miaka minne iliyopita kuandika kitabu kinachoainisha mawazo yangu juu ya Tanzania tuitakayo, Tanzania ya mabadiliko, Tanzania ya mapinduzi kuelekea kupata maisha bora kwa kila mtu. Ndani yake nimejaribu kuelezea, kwa kadri nilivyojaaliwa, jukumu la kizazi chetu ni nini haswa? Misingi ya ukombozi wa kiuchumi na kijamii ni ipi haswa? Nini chanzo cha umaskini na utajiri wa nchi? Nini kifanyike ili tuvune na kufaidika na utajiri tulionao? Nini vipaumbele na mbinu za ukombozi tunaoutaka sana sasa? Ni nini yanapaswa kuwa mabadiliko tunayoyatarajia? 

Katika kitabu hiki naweka mapendekezo ya mfumo mpya wa kuendesha uchumi kwenye nchi zinazoendelea za Afrika kutokana na misingi ya utamaduni asilia wa kiafrika, nazungumzia nguzo nane za mfumo huu, ambao nimeuita 'African Socialism with Capitalist Characteristics'. Kanuni hizi zilizosheheni muundo wa fikra zangu, uliwahi kuitwa 'Kigwanomics' na rafiki yangu Michael L. Wilson (Ph.D.) wakati tukijadili mambo mbali mbali ya kiuchumi na mustakabali wa Africa tunayoitaka akiufananisha na mawazo ya watu wengine mashuhuri duniani waliowahi kusimamia mabadiliko kwenye nchi zao na kufanikiwa, kama Ronald Reagan (Reaganomics) ama Thaksin Shinawatra (Thaksinomics). Nami nilipenda kuazima style hii na kukiita kitabu changu, Kigwanomics.  

Katika kitabu hiki utasoma uchambuzi wa mawazo ya waandishi mashuhuri duniani kama akina Mchumi Prof. Paul Collier (The Bottom Billion n.k.), Dr. Chika Onyeani (The Capitalist Nigger), Why Nations Fail (Drs. Robertson and Acemoglu), What went wrong with Africa (Roel van der Veen), Dead Aid (Dr. Dambisa Moyo), Towards the African Renaissance (Prof. Cheikh Anta Diop) na wasomi wengine wa Africa.  

Imani yangu ni kwamba nimetoa changamoto ya namna mpya ya kufikiria juu ya mapinduzi ya upili (Secondary revolution) kuelekea Tanzania iliyozaliwa upya (Tanzanian Renewal). Lengo kuu la mawazo yangu kwenye kitabu hiki ni hili. Kama ukisoma na ukaona upya wa mawazo yangu, na haja ya kuiunda upya Tanzania Tuitakayo basi nitakuwa nimefanikiwa. 

Kitabu kitazinduliwa rasmi taratibu zitakapokamilika na tutakujulisha. Nimeandika kitabu changu kwa lugha ya kiingereza, na tayari kuna timu, inayoongozwa na Ndg. Prince Bagenda, inafanyia kazi tafsiri ya kiswahili, na kuna wataalamu wanaofanya kazi ya kuandaa 'popular version' ya kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili ili kufikisha mawazo haya kwa haraka na kwa watu wengi zaidi. Ikikamilika kazi hii ndipo tutatangaza siku, mahala na saa ya kukizindua rasmi. Kwa sasa kinauzwa kwa bei ya 'promotion' ya TZS 5,000 kwa kila nakala, kwenye maduka ya TPH Bookshop na maduka yote ya Uchumi Supermarkets, Mlimani City (MAK Bookshop), pia kipo kwenye mikono ya wamachinga kwenye njia panda zote kubwa za jijini Dar es salaam, kimefika Iringa (Lutengano Investment), Vyuo Vikuu vyote iringa, Dodoma na Mwanza (Pia Kwa Ibrahim Campbell jirani na CRDB Mwanza Branch). 

Nakutakia usomaji mwema. Natanguliza Shukrani zangu za dhati na fanaka. 

Wakatabahu,
Hamisi Kigwangalla.
Mwandishi. 

"Vision is the ability to see the invisible!"
Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBA
P.O.Box 22499,
Dar es salaam.
Tanzania.
Phone No: +255 754 636963
                +255 782 636963
website: www.peercorpstrust.org or www.hamisikigwangalla.com
Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org or info@hamisikigwangalla.com
Skype ID: hkigwangalla
Blog: blog.hamisikigwangalla.com 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments