Lakini hapo hapo shule kadhaa za Seco nchini zinaendelea kufungwa na wanafunzi hasa wa kidato cha tano na vidato vingine vya chini kurudishwa nyumbani. Sababu inayotolewa kwa wanafunzi hao kurudishwa makwao ni kwamba HAKUNA CHAKULA!
Shule zilizotajwa kufungwa ni Tabora Boys' na Girls' secondary schools huko Tabora Region, Nsumba Boys' Secondary School, Mwanza, Masasi Girls' Secondary School na Ndanda High School huko Mtwara, Kahororo Secondary School huko Kagera na Songea Boys' Secondary School huko Ruvuma nk.
Ni jambo lisiloingia akilini kwa mwenye kufikiri; kuwa Tanzania tuna chakula tele, na kingine hata kuozea kwenye maghala huko Songea, Mbinga na Mbeya, Tanga nk kwa kukosekana kwa soko. Pia Chakula hicho kiko kwenye magala ya Serikali.
Kutokana utata huu, tuieleweje Serikali? Na Mawaziri wanaohusika wanasema nini kwa hawa wanafunzi wanaoathirika kikubwa hivi kielimu? Mimi sielewi. Labda mnisaidie wenzangu
Kessy
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments