[wanabidii] Fwd: SADFA

Sunday, April 05, 2015
>
> SADFA
> (Dr.Muhammed Seif Khatib)
> Mwanadamu ni zao la jamii.Jamii ina mambo ni vitu. Ili kurahisisha mawasiliano kila kitu
> kilichoumbwa au kutengenezwa na mwanadamu hukitambua na kukipa jina.Hakuna dhana
> au jambo litakosa jina la kuitwa.Lakini majina haya hayazuki na kuota kama uyoga.Kila
> jina la kitu,mtu,mimea au chama kina sababu zake na maana zake.Bila jina mahsusi mambo
> yangekuwa msegemnege.
> Mwaka 1956 na mwaka 1957 huku Zanzibar majina ya vyama vya siasa viwili
> yakabatizwa. Kimoja kikaitwa Zanzibar Nationalist Part, Subject of the Sultan.Nini
> maana yake? Chama cha Wananchi, Raia wa Sultan.Lakini kwa sababu viongozi wa
> chama hiki wengi wao walikuwa Waarab akina Ali Muhsin Barwani,Ahmed Seif Kharusi, Hilali Muhammed,Dr.Ahmed Idarusi Baalawi na Abdurahamnan Babu na wngine.Bila ya shaka kwa utashi wao uhusiano wao mkubwa na Sultn wa Kiarabu ikasadifu wakakita chama hiki jina sambamba na maana ile ya Kingereza na Kiswahili ya Hizbu El Watan
> Raiatul Sultan. Baadaye neno Subject of the Sultan kwa Kingereza na Raitul Sultan kwa Kiarabu na Raia wa Sultan kwa Kiswahil yakaachwa kutumiwa na chama hiki. jina pekee pekee lililoselelea ni kwa Kingereza la Zanzibar Nationalist Part kwa ufupi ZNP na kwa
> Kiarabu Hizbu. Jina la Chama cha Wananchi kwa maana ya Kiswahil halikutumka ingawa
> ndiyo tafsiri rasmi.Chama kingine kilichoundwa mwaka 1957 kikaitwa Afro,Shirazi Part.Maana yake chama cha Waafrika wenye asili ya bara na Waafrika(Washirazi)
> wenye asili ya Zanzibar.Ilisadifu kuwa katika nchi za jirani kuwa na majina yanayoonesha
> waziwazi kuwa ni vyama vilivyoundwa na Waafrika kwaajili ya kuwatetea Waafrika ndani
> ya bara la Afrika.Ilikuwepo Tanganyika Afirican National Union (TANU), Kenya Africa
> Union(KANU),African Nationa Congress(ANC).Neno 'African' lilitumika katika vyama vya siasa vingi katika bara la Afrika bila woga wala kumunyamunya maneno ama kuona
> aibu. Hii ilikuwa sadfa sio kama jina la 'Chama cha Wananchi' kijumla jumla na kukwepa
> kutumia 'African' au 'Chama cha Waafrika'.
> Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyoletwa na Afro- Shirazi yakafuta
> vyama vya siasa vya Umma Party,(Chama cha Umma), Zanzibar and Pemba People's
> Party((Chama cha watu wa Unguja na Pemba) na Hizbul el Watan(Chama cha Wananchi)
> vyote vya Zanzibar vilivyojitenga na neno 'African' katika majina ya vyama vyao. Hata hivyo, mwaka 1995 vyama vya siasa vikaruhusiwa kuanzishwa. Sheria ikakataza
> kutumia manjina ya vyama vya zamani vya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.Utii
> ukawepo.Hakuna TANU wala ASP! Hakuna UTP wa ZPPP,Umma Party wala
> Hizibu (ZNP).Hata hivyo imekuwa sadfa?Sadfa ya chama cha Zanzibar cha zamani
> chenye kutafsirika kuwa Chama cha Wananchi yaani Hizbu kimeibuka tena kujipenyeza
> katika siasa za sasa ingawa chambilecho kwa kibuyu kipya mvinyo wa zamani.Chama
> hakiongozwi na Ali Muhsin barwani,wala Ahmed Seif Kharusi au Dr.Ahmed Idarusi Baalawiy lakini fikira zao waasisi hawa haziko mbali kama mbingu na ardhi katika sera za
> msingi.Hizibu hawaisamehe Afro.Shirazi kwa kumtimua Sultn,kwa kufanikisha Mapinduzi
> na kuleta Muungano.Chama cha Wananchi cha sasa kinachofanana kwa jina kama Shillingi
> na rupia na chama cha Hizbu au ' Nationalist Party' kinayakubali Mapinduzi,kuyaenzi na
> kila mwaka kuyasherehekea? Matawi ya chama hiki hupambwa sheree zikifika? Kauli
> za viongozi kuyaenzi ya kuyatukuza zilitoka lini?Kauli za Hizibu na wafuasi wake siku zote
> wamekuwa wakiuabeza Mapinduzi na kutaka Mwungano huu uvunjike.Nini msimamo wa
> Chama cha Wananchi sasa kwa Mwungno huu? Si kuubeza tu ni kuuvunja kabisa kwa
> kutumia kaulimbiu 'Mamlaka Kamili' - nia ni kuuvunja Mwungano tunu ya Taifa letu.Lini
> vinywa vya viongozi wa Chama cha Wananchi wamesikika wakisema mavu na unyama na
> Usultan wa El Busaidy?Itakuwa ni sadfa kwa takribani wale waliokuwa wanachama
> na viongozi wa Hizbu ndiyo waniungayo mkono leo Chama Cha Wananchi? Naweza
> kuambiwa nitoe ushahidi! Hivi michango itoayo nje kusaidia Chama cha Wananchi kutoka
> nje intoka wapi? Nani anachangia na kwa nini? Viongozi wao wakienda nje ni nani
> wanawapokea na kukutana nao?Mitandao iliyoanzishwa ya watu walioghaibuni na
> wale waliohajiri nchi mielekeo yake inasemeje juu ya Mapinduzi na Mwungano?Tusiende
> mbali.Waswahili wanao msemo wao usemao,' Mtoto wa Nyoka ni Nyoka'. Afro Shirazi
> mwaka 1964 waliua nyoka na kuacha myai yake.Mayai yametotoa vitoto vya nyoka
> vimetokea na sumu kali kuliko ya wazazi wao.Wanataka waifute historia.Wafute
> Mapinduzi na wavunje Mwungano kupitia Hizbu ya leo ya Chama cha Wananchi.Kati ya
> mwaka 1957 na 1964 chaguzi nne zilifanyika Zanzibar chama cha Waafrika wa
> Zanzibar cha Afro_Shirazi kilikosa kura katika maneo ya Unguja na Pemba.Afro-
> Shirazi ilinyimwa kura Pemba yote ukiacha ushindi wa vuta nikuvute wa Mkoani na Chake
> tu. Waliowanyima kura Afro-Shirazi lakini wakawapa Hizbu ya zamani.Lakini leo
> Hizbu ya sasa ya Chama cha Wananchi inabebewa na wazee wachache na watoto na
> wajukuu wa Hizbu ya zamani.Nenda Unguja.Hizbu ya zamani ilikuwa inashinda Mji Mkongwe, Nungwi na Bumbwini.Hizbu ya sasa ya Chama cha Wananchi hawna ngome
> huko na kuishinda CCM ambayo ni Afro-Shirazi ya zamani?Nilipo chungua matukio na
> mfanano wa Hizbu (Chama cha Wananchi) cha mwaka 1956 na 1964 na kulinganisha Chama cha Wananchi cha mwaka 1995 na 2015 n akahitimisha kuwa hii ni sadfa. Nilipotafuta kamusi ya Kiswahili kutaka kujua maana ya neno sadfa nikaona maana
> Ifatayo.Sadfa:.Utokeaji wa mambo mawili kwa wakati mmoja bila kupangwa au
> kutarajiwa.Kwa tafsiri hii ni dhahiri Hizbu na Chama cha Wananchi vyama vinavyofanana
> kwa fikra na mawazo ya viongozi wao, hii ni sadfa? Malengo na sera ya vyama hivi ni sadfa?Nini hatima ya Mapinduzi na Mwungano kwa uwepo wa sadfa hii?
>
>
>
>
>
> Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments