Ambaye hakijui kisa cha mtoto mdogo kumuumbua mfalme kuwa anatembea uchi mbele ya watu wazima waliokuwa wanaogopa kumsema 'vibaya' mfalme anisamehe maana sitakieleza. Lakini ningependa kusema mimi katika utoto wangu nawaonyesha watu wazima habari za mfalme anayetembea uchi mbele zetu. Nadhibitisha kuwa mimi ni mtoto mdogo sana nilizaliwa saa 9 usiku wa kuamkia 5 September 1952 katika zahanati ya Kashasha. I am a young boy of 63 years now.
Mfalme mwenyewe ni watu hawa wazima walioitikia kwa kupotosha wito wa Rais wetu Dr. Jakaya Kikwete kuwa Inawezekana kumpata rais kwa kumshawishi mmoja wetu ambaye hata kama hataki lakini kama anaweza kunamshawishi.
Watanzania wote tunajua kuwa wapo wanachama wa CCM ambao wanatumikia adhabu ya kuangaliwa mwenendo wao baada ya kuonekana wanapiga kampeni ya kugombea uRais kabla ya wakati. Waliofungiwa kufanya hivyo ni pamoja na waziri Mkuu aliyejiuzuru kwa Kashfa Mpendwa wetu Edward Lowasa, Benard Membe, January Makamba, Wasira na kadhalika.
Moja kati ya matendo waliyokuwa wanafanya ni kujipitisha kwenye makanisa na misikiti kujidai wanatoa michango. Watu wenye akili wakatafsiri matendo hayo kuwa ni rushwa ya kutaka waungwe mkono wakati wa kugombea urais
Tamko la rais kuwa tunaweza kumshawishi mmoja wetu ambaye japo hajajitokeza na labda hataki kujitokeza bila shaka yoyote kwa mtu mwenye akili za kawaida (kila mtu ana akili lakini si kila mtu anzo za kawaida) anajua kuwa rais aliowasema sio wale waliokwisha kujitokeza na kuonyesha nia ya kuutaka urais mpaka kufikia hatua ya kufungiwa kuutaka urais. Haiingii akilini.
Kitu cha ajabu na cha kushangaza watu wazima, viongozi wa dini eti wameenda kumshawishi mwenzetu Edward Lowasa, 'kumuomba' 'akubali' kugombea urais. Haiingii akilini katika maeneo mengi.
Tuanzia hapa:
i Yapo maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond ambayo nadhani hayajatekelezwa na serikali. Kama yakitekelezwa huwezi kujua kama hayawezi kudhibitisha uchafu wa wahusika akilwemo Lowasa wetu.
ii Kashfa muhimu na kubwa ni kuwa capacity charges zilizotamkwa ndani ya ripoti ya tume ya bunge ina mgao wa wahusika na haijulikani kama EL hayumo
iii Katika michango ambayo EL alikuwa akitoa makanisani misikitini na kwingineko inadhaniwa kuwa huenda sehemu yake inatokana na mgao huo.
iv Kulionekana dalili kuwa kuna mambo tume ya Bunge chini ya Dr. Mwakyembe ilibakiza mambo fulani ambayo ingeyatoa kuna watu wangepata shida. Tunakumbuka aliposema aliwahi kufuatwa na mke wa mtu fulani kumsihi afiche ukweli wa ripoti. EL hakuacha kutajwa katika hilo.
V Na kadhalika.
Taifa letu lina matatizo makubwa sana. Mengine ni nyufa alizozieleza Mwalimu Nyerere mwaka 1995. Sasa zimemeguka na kuwa kubwa zaidi. Rushwa sasa imezidi na kupata jina advanced tunaiita UFISADI.
Kila mwenye akili timamu yuko anaumiza kichwa akitaka kujua tufanyeje ili tupate kiongozi bora na tumjueje ambaye si fisadi. Kila mwenye akili sawasawa anajua kuwa aliyekwisha tajwa kwa hilo hafai hata akitaka kutumia njia zake kuupata urais.
Sasa katika mazingira hayo:
1. Viongozi wetu ambao walikuwa wakipokea michango hiyo haramu wajisafisheje mtu akisema walinunuliwa na kuandaliwa kwa wakati kama huu?
2. Viongozi wetu hao wana upeo kiasi gani kukubali kutumiwa kihuni namna hii? Kweli walilenga kwenda kumshawishi Lowasa agombee kwa sababu wameona amekaa kimya yaani hafurukuti kugombea? Yaani viongozi wetu walidhani hawatajulikana kuwa lazima wamehongwa kufanya kazi hiyo?
3. Wanaweza kusimama na kujitetea mbele ya waumini wao kuwa walifikiri Lowasa hatajitokeza kugombea ndiyo maana waliamua kumshawishi na kumchangia fedha? Wameona wamejitokeza wangapi mpaka wakahofu kuwa huenda asijitokeze?
4. Wanataka Lowasa aje alisaidie taifa hili kufanya nini? Wanaona taifa halina nini? Wengine tunaona taifa ni tajiri, Lina raslimali, lina watu wapole waelekevu. Shida linakosa kiongozi wa kuukabili ulafi na kujilimbikiza mali ili mali iliyopo itumike vizuri. Kweli mtu mwenye kashfa ya namna iliyo kwenye ripoti ya Tume ya Bunge anaweza kupendekezwa na viongozi wa dini? Hii balaa. Viongozi hao ambao ni waombezi wa Taifa hili kweli wana dhamira njema?
Siwaelewi. Viongozi hawa wamejua jinsi ambavyo Lowasa ameleta mgogoro katika viongozi wa kimila wa kimasai? Na kuwa mgogoro huo ni uimla wa kutaka kuwabambikizia wanaMonduli mtu anayetaka amrithi ubunge yeye atakapo kuwa rais? Ndiye wanayetaka aongoze taifa hili?
Lowasa anaweza kuwa rais lakini nafikiri viongozi wa dini wasingependa kuwa sehemu ya waliomsaidia. Lowasa amesemwa sana. Kwa hiyo anaweza kuwa rais na akawa mzuri sana hivyo kutukomesha tunaomsema. Lakini akiwa mbaya kuna atakayeshangaa?
Rais Kikwete alipoupata urais wakati watu wakitabiri nani atakuwa waziri Mkuu wapo waliomtaja Lowasa. Wako waliosema haiwezekani akawa Lowasa. Sababu zilikuwa kwa sababu ni rafiki wa JK basi (JK) atashindwa kumdhibiti. Waliosema anaweza kuwa Lowasa walisema atajitahidi kutomudhalilisha rafiki yake? Nini kilitokea? Unawezaje kumwamini Lowasa? Mimi nawashangaa viongozi wa dini . si viongozi wa siasa wa chama chake. Hayo tumeyazoea. Mitandao ilikotufikisha ni wao hakuna zaidi. Siwashangai wanafunzi. Wao ndivyo wameelekezwa na wanamtandao na ni haki yao. Wanakomea hapo. Siwashangai vijana wa bodaboda. Hao tumewazoea. Tunawakuta wakishajaziwa mafuta ya pikipiki zao basi. Nini zaidi. Lakini viongozi wa dini???? Nitaendelea kuwashangaa.
Elisa Muhingo
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments