[wanabidii] Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni walipoliweka jiji la Stuttgart chini yao !

Wednesday, March 18, 2015







FFU-Ughaibuni aka Viumbe wa ajabu "Anunnaki" wafanikiwa kulituliza jiji la Stuttgart

 (Picha kwa hisani ya issamichuzi.blogspot ),

Bendi Maarufu ya Muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni usiku wa Jumamosi ya 14 Machi 2015 walifanikiwa kufanya  mavitu yao jukwaani na kuliweka jiji la Stuttgart,chini ya himaya na muziki wao.katika onyesho hilo la Africa Unite Party , ulinzi ulioandaliwa katika onyesho lakini kikosi kazi Ngoma Africa band kilikuwa "Fit on Fire" , walisindikizwa jukwaani na askari maalumu wa ujerumani,lakini cha kushangaza wanamuziki wenyewe walikuwa katika mavazi ya ubaya ubaya ! kwa kuwa sheria za ughaibuni zinawaruhusu kutinga na viwalo..kila nchi inautaratibu na sheria zake ,wadaku wanatonya kuwa
bendi hiyo maarufu ilikuwa na ujumbe sio kila anayevaa viwalo vya ubaya ubaya au wajeda ni mvunja amani au mpenda vita bali anaweza kuwa mpiga gitaa badala ya mtutu "Peace for All",washabiki wengine walidai kuwa Ngoma Africa band walikuwa wanawachimbia mkwala baadhi ya vijana wa kijerumani 'Neo Nazi" wenye tabia za kuvamia wageni ambao pamoja na kuwapo ulinzi katika onyesho lile lakini labda wangeweza kupenya.
wasikilize at www.ngoma-africa.com



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments