(a)Jinsi ya kujiandaa na mahojiano (Interview)
Kuna hatua zifuatazo ambazo unatakiwa kuzifuata kwenye mahojiano;
1.Kuelewa nini maana ya mahojiano
2. Jinsi ya kujiandaa na mahojiano
3.Jinsi ya kufanya vizuri katika mahojiano
4.Namna ya kufuatilia baada ya mahojiano
(b) Nini maana ya mahojiano
Mahojiano ni njia ya kukutana na kufahamiana kati yako na mtu anayekufanyia mahojiano yaani mwajiri na jopo lake la mahojiano. Pia ni fursa ya kuonyesha hatua chanya kuelekea kuendeleza taaluma yako. Uzoefu kazini na elimu yako si kigezo pekee cha kuonyesha kuwa wewe ni mtu sahihi kuajiriwa. Matokeo mazuri ya mahojiano ni jinsi utakavyoweza kujieleza.
Jee madhumuni ya mahojiano ni yapi?
Mahojiano ni njia ya mwajiri ya kuchagua mwombaji ajira sahihi toka kwa waombaji wenye sifa zinazolingana ambapo mchujo utasababisha mshindi kupata kazi.
Yafuatayo hapa chini ni madhumuni ya mahojiano;
1. Mwajiri anataka kujiua kama wewe unafaa kwenye kampuni/taasisi yake. Anataka kujua mambo matatu;
– Jee unaweza kuifanya kazi yake?
– Jee utaifanya kazi yake?
– Jee utamfaa?
2. Unataka kujieleza na kumshawishi mwajiri kwamba unafaa kuajiriwa na unataka kujua kama Kampuni itakufaa katika kuendeleza taaluma yako.
3. Mahojiano ni fursa ya kuonyesha ujuzi na uzoefu wako katika kazi unayoiomba. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuonyesha katika mahojiano;
– Kujitambulisha
– Kuonyesha ujuzi wako kwa kujibu maswali ya kitaaluma yanayohusiana na kazi uliyoomba, yanaweza kuwa ya kujibu ana kwa ana au mtihani wa maandishi.
– Eneo gani uko imara
– Una mapungufu gani
– Ni jinsi gani unaweza kuifanya kazi
– Unataka kufanya kazi kwenye kampuni kwa muda gani?
– Nafasi hii inakufaa vipi?
– Kwa nini unataka kuhama huko ulikotoka na kujiunga na kampuni mpya?
4. Mahojiano ni sehemu ya kuangalia kama hiyo kampuni ni mahali sahihi kufanya kazi. Mambo yafuatayo unapaswa kuyaangalia;
– Jee hii ni sehemu unayotaka kufanya kazi
– Jee utatoa mchango wako kikamilifu?
– Jee kuna fursa ya kujiendeleza na kupata ujuzi mpya?
(c) Mambo ya kufanya kabla ya mahojiano.
Yafuatayo hapa chini ni mambo ambayo unatakiwa kuyafanya kabla ya mahojiano.
– Kusanya habari kuhusu kampuni inayotaka kukuajiri.
– Andaa mpango wa jinsi utakavyokwenda kwenye mahojiano ikiwa ni pamoja kuwa na orodha ya wadhamini ukitakiwa kutaja wadhamini.
– Jiandae na mavazi utakayovaa siku ya mahojiano. Vaa nguo safi ya heshima iliyopigwa pasi, kiatu kilichongarishwa na kiwi na soksi safi. Usivae jeans, nguo ya kubana nguo za michezo, vitop au Tshirt nguo hizo haziruhusiwi sehemu za kazi zinaweza kukukosesha kazi na kuonekana mhuni.
– Jiandae na mahojiano hasa katika mambo yafuatayo; Uzoefu wako kazini kama umewahi kufanya kazi kama unayoomba,elimu yako,ujuzi ulionao kama vile umekwenda chuoni ukasoma na kupata cheti au Diploma na Digrii ya uhasibu nk. Ufahamu wako kuhusu kampuni unayotaka kuajiriwa nayo, mipango yako ya kujiendeleza, mambo gani umeshafanya au malengo yako binafsi uliyokuwa umejiwekea umeyatimiza? Vitu gani vinakuvutia, mshara na marupurupu. Jiandae kujibu maswali yanayohusiana na taaluma yako kama unaomba kazi ya uhasibu jiulize kazi za mhasibu ni zipi pitia topic za (definition) maana ya neon mhasibu, kazi zake ni zipi, changamoto zinazoweza kukukabili kazini nk.
– Andaa majibu ya maswali yaliyoyatajwa hapo juu.
– Fanya mazoezi ya jinsi ya kujibu maswali kwa kujiangalia kwenye kioo au mtafute mtu wa kukuuliza maswali na wewe ujibu.
– Fanya mazoezi jinsi ya kujitambulisha. Mfano mimi ni Charles Paul ni kijana mwenye umri wa miaka 21 nimesoma hadi kidato cha sita, nina Diploma ya uhasibu toka chuo cha Biashara CBE. Sasa hivi ninafanya kazi ya Mhasibu msaidizi Kampuni ya ya Matunda LTD. Nina uzoefu kazini wa miaka 5 kazini.
– Unatakiwa kujua ilipo ofisi utakapokwenda kufanya mahojiano.
– Unatakiwa kuwahi kwenye mahojiano, ufike angalau saa 1 au nusu saa kabla ya muda wa mahojiano hali hii itaonyesha kuwa uko makini.
(d)Mambo ya kufanya wakati wa mahojiano
Kuingia kwenye mahojiano.
Wakati unaingia kwenye chumba cha mahojiano jiamini, unyesha uchangamfu na uwe mwenye furaha. Waangalie watu machoni na uwasalimie kwa kuwapa mikono kama fursa hiyo ipo. Hapa ndipo umuhimu wa kuwa msafi unatakiwa, unapaswa kuwa na nguo safi za heshima na zimepigwa pasi, umepiga mswaki, nywele na ndevu zimekatwa na kuonekana u nadhifu.
Mara nyingi mwajiri atajitambulisha kwako na kwa wanajopo waliopo. Pia watakutaka ujitambulishe. Kisha wataanza kukuliza maswali.
Maswali ambayo unaweza kuulizwa ni kuhusu;
– Ufahamu wako kuhusu kampuni unayotaka kuajiriwa nayo.
– Kwa nini unataka kujiunga na kampuni hiyo?
– Kwa nini unahama.
– Unafahamu nini kuhusu nafasi ya kazi unayoiomba, kwa mfano kama unaomba kazi ya uhasibu, utaulizwa nini maana ya mhasibu kazi zake ni zipi. Unaeza kuulizwa kwa undani ukapewa maswali ya mtihani wa maandishi kuhusu topic Fulani kwa mfano bank reconciliation, kusahihisha makosa kwenye vitabu vya mahesabu nk.
– Unaweza kuulizwa kuhusu habari zinazoendelea duniani au nchini (Current affairs)
– Ni eneo gani uko imara
– Mapungufu yako ni yapi
– Ukipewa kazi unahitaji mshahara wa kiasi gani.
– Ukipata kazi unaweza kuanza lini. Jibu ni mara moja.
– Unaweza kupewa fursa ya kuuliza maswali. Uliza maswali kutaka kujua zaidi kuhusu ufafanuzi wa mambo muhimu na uelewa wako kuhusu kampuni.
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kufanya mahojiano.
– Unatakiwa kuwa msikilizaji mzuri usimkatishe mtu kwa kuingilia swali kabla hajamaliza kuuliza.
– Fuatilia kwa umakini kile kiachoulizwa.
– Uwe na utulivu.
– Ujiamini ila usijiamini kupita kiasi.
– Zungumza taratibu na kwa utulivu.
– Mwangalie muulizaji swali machoni usiangalie pembeni au kuinama.
– Uwe huru.
(d)Mambo ya kufanya baada ya mahojiano
Baada ya mahohiano mtafahamishwa kuhusu utaratibu mtakaofanyika kukufahamisha kama umepata kazi au hujapata kazi. Si vyema kumfuatilia mwajiri kwa simu au kwenda ofisini kuulizia kuhusu majibu ya mahojiano, ni vyema ukasubiri kufahamishwa kama umefanikiwa kupata ajira au hapana.
Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa Kampuni ya CPM Business Consultants, Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa kujiunga;http://tinyurl.com/mshauriwabiashara au Piga simu namba 0784394701
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments