MBINU CHAFU ZA MEMBE ZAVUJA
Duniani hakuna siri na kila ukifanyacho Duniani lazima Walimwengu watakuona. Ilikuwa ni juzi mida ya jioni maeneo ya Serena Hotel walikutana na anayejifanya afisa usalama wa Taifa Jack Gotham, Waziri wa Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe pamoja na mtoto wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete kwa ajili ya kupanga namna ya kuanza kampeni za urais kwa kutumia migongo ya vijana.
Membe ambaye ana tajwa tajwa kugombea urithi wa Rais Kikwete mwaka huu alikutana na Ridhiwani, Jack Gotham pamoja na mwanamke mmoja siku ya Jumanne tarehe 10/3/2015 saa 1 usiku na kufanya kikao cha siri cha kufanya kampeni za urais kwa kupanga kuanza kwa kufanya kongamano kuhusu madawa ya kulevya pamoja na ukimwi siku ya Jumatano ya tarehe 18/03/2015.
Habari zaidi zinadai kongamano hilo wamepanga kuwashirikisha wanafunzi wa vyuo vikuu, watu kutoka taasisi mbalimbali na wananchi wa kawaida na kumwalika Mhe. Bernard Membe anayetajwa tajwa kugombea urais ili awe mgeni rasmi.
Lengo mficho la kongamano hilo ni kuanza kampeni za chini kwa chini huku Membe akidai kupata nguvu na Baraka zote za kuanza kampeni hizo toka kwa ngazi za juu zilizo wakilishwa na mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete. Membe ambaye ni mtoto wa nje wa Mzee Mrisho Kikwete amekuwa akiungwa mkono mara zote na familia ya Rais Kikwete kupitia mwanae Ridhiwani Kikwete pamoja na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika harakati za kisiasa hususani mbio za Urais.
Kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe 18/03/2015 limeandaliwa mahsusi kwa ajili ya kumjengea umaarufu na kubaliko la Membe kwa vijana wa vyuoni ambako hakubaliki kabisa na wasomi hao na bajeti iliyotengwa kwa ajili ya kongamano hilo ni milioni 500 huku ikijumuishwa pamoja na kuwapa shukrani ya laki moja moja kwa wale wote vijana watakaoshiriki katika kongamano hilo.
Na hivi sasa pesa zimeshaanza kumwagwa mavyuoni kwa ajili ya kuwashawishi wanafunzi wa vyuoni kushiriki kongamano hilo ambapo wasimamizi wa kila vyuo wameambiwa ni lazima wahakikishe wanapata washiriki wa kongamano hilo kwani ni agizo toka ngazi za juu.
Ikumbukwe Bernad Membe pamoja na makada wengine sita wa CCM wamefungiwa kwa takribani mwaka mzima na vikao vya juu vya CCM kutokana na kuanza kampeni za urais mapema na mpaka leo hii bado wapo kifungoni lakini Membe ameshaanza kupanga mbinu za kutokutii adhabu hiyo ya kifungo hicho kwa kupanga kuanza kufanya kongamano ambalo lengo lake kuu la chini kwa chini ni kufanya kampeni za urais.
Walihitimisha kikao hicho kwa kukubaliana yeyote yule atakaye kwamisha ama kutokushiriki tukio hilo watawashughulikia ipasavyo kwani ni uamuzi uliotoka juu.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments