HAYA NI MAONI YANGU NA USHAURI WANGU BINAFSI YASIHUSISHWE NA KAZI AU SHUGULI ZANGU ZOZOTE .
Watu au jamii ambayo inakaa eneo Fulani kwa muda mrefu kwa nia ya kuja kufanya uhalifu siku zijazo kama walivyoapa baada ya kuambiwa wanaitwa SLEEPER CELLS – Sleeper ni neno la kiingereza lenye maana ya mtu aliyelala , CELLS ndio vikundi vyenyewe na pale anapoambiwa kuanza kazi anakuwa ACTIVATED .
Kwahiyo inawezekana hawa wahalifu walilala kwa kipindi kirefu wakikusanya taarifa , silaha , watu na mambo mengine kabla ya kuanza shuguli yenyewe ambayo walitakiwa kupewa maagizo na wakubwa zao ambao inawezekana wako nchini au nje .
KUNA MAMBO MAWILI KWENYE SUALA HILI .
Kabla ya kuangalia tukio la sasa tukumbuke miaka ya 70 wakati IDDI AMIN wa Uganda alivyopindua serikali ya Obote na kuanza uchokozi dhidi ya Tanzania ahadi yake ilikuwa ni kufika mpaka Bandari ya Tanga aliamini akiteka bandari hiyo itamsaidia kuvusha mizigo na mengine kwenda Uganda na maeneo ya mbali zaidi .
Pili kuna mrafi wa Bandari na Njia ya Reli ya Tanga ambao lengo ni kufika maeneo ya kati na nje ya Tanzania ambao sijajua nani wanaufadhili , mradi kama huu uko Kenya maeneo ya Lamu ambao unaunganisha nchi za Ethiopia , Uganda , Sudani Kusini na Kenya ambapo kumekuwa na mapigano ya alshabaab na wahalifu wengine mbalimbali .
Inawezekana virugu hizi zina lengo la kuzuia mradi wa Tanga dhidi ya miradi mengine ya nchi jirani au wale waliopewa mradi wenyewe wako kwenye ushindani na mataifa mengine yaliyokosa mradi na kukosa fursa na malengo mengine ya muda mrefu .
Hivi ni vitu vyote vya kuangalia na kuvifanyia uchunguzi mzuri na wa muda mrefu ili kujihakikishia usalam wetu na wa watu wetu .
Sasa twende kwenye suala lenyewe la Magaidi katika mapango karibu na Amboni Mkoani Tanga .
SUALA LA MAPANGO KARIBU NA MAPANGO YA AMBONI
Mtuhumiwa aliyewapeleka Askari hapo kwenye eneo alitumbukia kwenye Pango .
Baadaye muda wa saa 7 usiku askari walishtukizwa kwa kushambuliwa na risasi na milipuko mengine toka kwenye mapango .
Baadhi ya askari walijeruhiwa kwa sababu hawakuwa na vest za kuzuia risasi kwa muda ule walikimbizwa hospitali .
Askari waliofika mwanzo walitaka kulipua mapango na mahandaki mengine kwa ajili ya kusawazisha eneo husika baadaye ikatoka amri ya kukamata watuhumiwa wote wakiwa hai .
Kuna matatizo kadhaa yamejitokeza kutokana na suala hili .
1 – Askari wote polisi , jeshi na wengine wanatakiwa siku zote wawe na tahadhari kutokana na matukio yanayoendelea haswa ya kuumiza , kuuwa na kuvamia vituo vya polisi , walioenda na mtuhumiwa walitakiwa wawe na tahadhari zote hizi kwamba wangeweza kuvamiwa hata waliofuatia walitakiwa kujua .
2 – Kabla ya kwenda eneo au kumfuata mtu hatari kama hawa inatakiwa assessment kujua zaidi kuhusu mtu mwenyewe alipotokea , jamaa zake wengine wa karibu , mafunzo aliyonayo na uwezo wake mwingine . Kama alikuwa na mafunzo ya kijeshi na imeonekana hivyo kutokana na mahojiano basi ingetakiwa nguvu ya kumpeleka eneo la tukio na nguvu zaidi ya kuvamia eneo husika kwa ajili ya kukamata wengine wote .
Lakini pia kama mtuhumiwa ana ndugu au jamaa zake wakaribu wangeweza kutumika hao kumshawishi au kutumia njia nyingine kupata taarifa zaidi kuhusu mtuhumiwa na watu wake wa karibu kwahiyo wakati anapelekwa pangoni wengine wangeenda kusaka wengine zaidi .
Kama upelelezi wa mambo kama haya ndugu , marafiki na watu wa karibu wa watuhumiwa ni muhimu sana katika kusaka suluhu au kupata kile kinachotakiwa .
Suluhu kwa maana mtuhumiwa au watuhumiwa wanaweza kuamua kujisalimisha bila kufanywa chochote kwa ahadi ya kutoa taarifa zote walizonazo pamoja na wenyewe kupewa hifadhi na kutekelezewa madai mengine .
UTUMIAJI WA VIFAA VYA KISASA VYA MAWASILIANO NA PICHA
Taarifa zilizopo zinasema askari walianza kushambuliwa usiku kutoka mapangoni kisha baadhi wakatoroka kupitia matobo mengine kwenye mapango hayo hayo .
Kama ni usiku askari wangekuwa na vifaa vya kuona usiku na mawasiliano mengine ya wireless badala ya radio call ambazo mtu angeweza kuvaa na kuendelea na shuguli bila wasiwasi wowote na inawezekana vitu kama hivi magaidi wanavyo na ndio maana ilikuwa rahisi kwa wao kutoroka na kutokomea huku wakijua wanakoenda .
Pia ingeweza kutumia DRONE kwa ajili ya kupiga picha eneo husika kutokea angani na maeneo mengine yote ya msitu bila ya askari kufika na kama wakifika basi waendele kwa maelezo kutoka kwa wale wanaosoma na kutafsiri picha za drone na kuwatumia wale walio chini wanaoendelea na harakati za kutafuta au kupambana na watuhumiwa husika .
DRONE nyingi zinauwezo wa kuruka kwa ajili ya kupiga picha au kufanya mashambulizi kwa saa zaidi ya 24 usiku na mchana bila kushambuliwa au kuonwa kwa urahisi .
Baadhi ya nchi ndio zimeanza kufanya utafiti kuhusu utengenezaji wa silaha na vifaa vingine vya kupambana na DRONE kwenye anga zao kwa sababu zinatengenezwa nyingi na hata baadhi ya makundi ya kigaidi wanazo na wamewahi kuzitumia mara kadhaa kwenye hujuma au kutafuta taarifa wanazohitaji kabla ya kushambulia .
WASEMAJI WA JESHI NA SERIKALI
Naamini Vikosi mbalimbali vya Jeshi mkoa wa Tanga vina wasemaji wake ambao wanajua eneo husika vizuri pamoja na mambo mengine mengi .
Siku nyingine ni vizuri kutumia hawa wenyeji katika kutoa taarifa zinazohusu matukio kwenye maeneo yao , hawa wamezoeleka na wananchi na wanaijua jamii yao vizuri zaidi kuliko wale wa makao makuu au wale wakuu kabisa ambao wanategemea taarifa kutoka kwa watu hawa .
Hii itarahisisha ufafanuzi wa baadhi ya maswali na majibu endapo ngazi ya mtaa , wilaya , au mkoa ikikosea basi makao makuu watakuwa na majibu mazuri zaidi kuliko kupata majibu kutoka makao makuu moja kwa moja na kuruka hawa wengine .
UPANDE WA SERIKALI
Ihakikishe maeneo nyeti au maeneo yenye migogoro au mashaka ya kiulinzi na usalama viongozi wa huko kuanzia mitaa , vitongoji , wilaya na Vijiji wanateuliwa kutokana na mafunzo na mbinu nyingine watakazopewa ili waweze kutambua , kuhoji na kufuatilia vitu hivi kwa undani na kutoa taarifa kwa wahusika .
WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA
Tumeona baadhi ya mashirika ya kimataifa yakitoa watu wao kwa ajili ya kujitolea kwenye maeneo mbalimbali nchini na kutembelea maeneo mengi tu bila ya wenyeji wao kujua au kuwafuatilia sasa huu uwe mwisho .
Mtu yeyote anayekuja nchini kwa ajili ya shuguli za kujitolea atoe taarifa za kote anakoenda au anapopanga kwenda na ikiwezekana aende na mwenyeji wake sehemu zote na kama alipiga picha basi nakala zibaki kwa wenyeji .
USHAURI
Kuna umuhimu wa kuondoa vikosi vya ulinzi kwenye vyama vya siasa na hata wanaposhiriki kwenye kampeni basi walinzi wawe wa serikali na sio vyama vya siasa labda kuwe na sababu maalumu na muhimu .
Vyama vyote vya siasa vipeleke orodha ya watu wote waliomo kwenye vikosi vyao vya ulinzi na aina ya mafunzo walioyopokea au wanayoendelea kupokea ndani na nje ya nchi hata wale waliofukuzwa au kuhama vyama au kufariki kwa sababu zozote zile .
Inawezekana baadhi ya wahalifu walipata mafunzo kwenye vyama vya siasa au sehemu nyingine wakafukuzwa au wakahama vyama au wakajiondoa wenyewe huku wakiwa na hazina ya ujuzi na utaalamu wa aina mbalimbali ambao wanautumia kwenye shuguli haramu kama hizi .
MWISHO
Nawapongeza wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika shuguli hii mpaka ilipofikia naamini baada ya muda wahusika wote au wale muhimu watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake .
Pia nawapa pole wale wote walioumizwa kwa kupoteza ndugu , jamaa , marafiki na mali kutokana na shuguli hii .
YONA FARES MARO
0786 806028
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments