[Mabadiliko] DC KUSHUSHA VYEO WALIMU NA KUSEMA WENGINE WACHUKULIWE HATUA ZA KINIDHAMU

Tuesday, February 17, 2015
Gazeti la mwananchi lina habari ya mkuu wa wilaya huko Geita amependekeza halmashauri iwachukulie hatua walimu walio hamasisha wanafunzi kufunga barabra wakilalamikia kutokujengwa kwa matuta.
Nashindwa kuelewa kiwango cha uelewa wa mkuu huyu wa wilaya, na ama kama ni kweli anayafanya haya akimwakilisha rais au ni hujua wake.

Wanafunzi walikuwa wanalilia mwenzao aliyegongwa wakati akivuka. Inawezekana shule ipo karibu na barabara. Pia shule hiyo itakuwa imejengwa na serikali. Tena waliokwisha kugongwa ni wengi sana, na pia ombi la kujengwa matuta lilitolewa siku nyingi.
Twende sasa tuangalie uelewa wa huyu mwakilishi wa rais wa nchi hii.
Ukipata msiba hasa wa mtu unayemjua au unadhani ni mnyonge ama unayeshawishika kumwonea huruma utulivu hupungua. kisaikolojia hutokea kutokuikubali hali hiyo, kuogopa, kujilaumu au kulaumu na wakati mwingie mshtuko wa kuzimia.
wanafunzi wakiwa kwenye hdhuni waliona bora tufe wote. Waliojenga shule karibu na barabra ndiyo vyombo vyao vya moto vinatuua, tena hawatusikilizi. wapita njia na waliokaribu na barabara wamechoka kuona vifo vinavyoumiza.
Wametafuta njia ya kuongea masikio haya sikii.
Walimu hawana ubavu wa kuzuia watoto waliochanganyikiwa. tunazungumzia watoto wenye miaka kuanzia 7 - 20 na wao wapo kama 2000 dhidi ya walimu 30 na mlizni mmoja.
Jitu moja pumbavu linakuja na kusema eti hatua za kisheria na wapunguzwe au kushushwa vyeo. hayawani mkubwa huyu.
Najiuliza amefanya utafiti lini mpaka akajua kuwa walihamasishwa na siyo msukumo wa hisia/ mihemko?
Mbona bosi wake akikamata mtu na fedha ya umma anafanya uchunguzi? au tuelewe ndiyo alivyotumwa na bosi wake kuwa wakifa watoto wa kayumba yeyote anayeomboleza piga mabomu na fukuza kazi? Inamaana anachokifanya kina Baraka ya aliyemteua? Amewahi kujifunza baada ya kifo ni hatua gani mfiwa hupitia kabla ya kuwa katika hali ya kawaida?
MKUU WA WILAYA NAKUCHUKIA kuliko shetani!!!!!!

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com


For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1424172305.89810.YahooMailBasic%40web160305.mail.bf1.yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments