[wanabidii] VIONGOZI WA MAKANISA WAHITAJI UONI MPANA WA KISIASA

Saturday, January 03, 2015

Kumb: 07/1436 AH Jumatatu, 07th Rabii I 1436 AH 29/12/2014 CE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

VIONGOZI WA MAKANISA WAHITAJI UONI MPANA WA KISIASA

Kufuatia maadhimisho ya Sikukuu ya X-mass takriban Viongozi wote wa Makanisa kutoka madhehebu mbali mbali nchini Tanzania katika mikusanyiko ya ibada zao wameangazia suala la Kashfa ya unyakuaji wa Sh300 billioni inayojuulikana kwa jina la Tegeta Escrow Account (TEA)

Hatua hiyo ya Viongozi wa Makanisa ni dhihirisho la wazi la hisia zao kwa machungu ya kusheheni na kuota mizizi kwa matendo ya rushwa, ubadhirifu, na kila aina ya ufisadi iliyokita ndani ya nidhamu ya kidemokrasia. Kama kila siku kunavyochipuka shehena ya kashfa zisizomalizika. Mifano hai kama vile kashfa ya Richmond, kashfa ya EPA (External Payment Arrears) in 2005/2006 wahusika wakiwa na kampuni ya mkobani walikwapua zaidi ya Sh133 kutoka akaunti ya Kitengo cha Benki Kuu cha malipo ya nje (EPA). Kisha waporaji hao kwa unyenyekevu na kwa ridhaa zao wakatakiwa warejeshe fedha hizo bila ya kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria kwa waliotii mwito huo. Pia kuna kashfa ya Ununuzi wa Rada kwa bei ya ziada ya kidanganyifu ndani ya mwaka 1999. Baadae ikagundulikana thuluthi moja ya malipo ya ununuzi wa Rada hiyo yaliingia mfukoni mwa tapeli raia wa Uingereza aliyefanikisha ununuzi huo.

Sauti za majonzi za Viongozi wa makanisa dhidi ya wanasiasa waovu wa kidemokrasia waliohusika na kashfa kama ya Escrow ni dalili tosha kuwa mwanadamu huzaliwa na maumbile ya ndani ya kisiasa. Yaani ana msukumo wa ndani wa kujishughulisha na kuyasimamia masuala yanayogusa maisha yake na maisha ya wengine. Hii inatokana na hisia ya kimaumbile ya mwanadamu kutaka kuhifadhi na kuendeleza maisha yake kwa utulivu na furaha. Kinyume kabisaa na mafundisho ya kimakosa ya kanisa yanayohubiri msimamo wa kisekula usemao: 'Mpe Mungu kilicho cha Mungu, na mpe ya Kaisari kilicho cha Kaisari'. Pamoja na mafundisho hayo ya kisekula ambayo ilipaswa ndio iwe dira ya kanisa, bado mara nyingi tunawaona viongozi wa makanisa hukhalifu mafundisho hayo na hujihusisha na siasa kwa kukemea uovu na ufisadi unaotendwa na wanasiasa wa kidemokrasia.

Kwa msingi huo sisi Chama cha Kiislamu cha Hizb ut-Tahrir tunapenda 
kuwakumbusha Viongozi wa Makanisa na wanaojitenga na siasa, kwamba siasa ni sehemu ya maumbile ya mwanadamu na hakuna namna ya kuiepuka.

Lakini mabadiliko ya kweli yatafikiwa tu kwa kuondoa mfumo muovu wa kibepari uliopo kwa mbadala wa mfumo wa Uislamu na nidhamu yake ya kiutawala ya Khilafah. Kwa bahati mbaya Kanisa daima huzingirwa na mtego wa mfumo wa kibepari. Huku baadhi ya makanisa amma hubakia kupakapaka mafuta na kunyamaza kimya dhidi ya dhulma za wanasiasa wa kidemokrasia au wanapokemea, hutoa mwito wa mabadiliko ndani ya nidhamu hiyo hiyo thaqili badala ya kufanya kazi kukomesha kabisa mfumo wa kibepari kutoka katika msingi wake.

Muda muwafaka umewadia kwa Viongozi wa Makanisa na wanafikra jumla kutafiti mfumo bora mbadala, ambao hapana shaka si mwengine zaidi ya Uislamu, kama kweli wana dhamira ya dhati ya kuutetea umma na kuwakomboa 
wanadamu kutokana na makucha ya dhulma yaliyojaa damu ya mfumo wa kibepari na nidhamu yake ya kiutawala ya kidemokrasia ishayoshindwa wazi wazi na kushuhudiwa na kila mtu.

﴿قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَى كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلاَّ نَعْبُدَ إِلاَّ اللَّهَ وَلاَ نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلاَ يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِنْ دُونِ اللَّهِ فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ﴾ [آل عمران: 64]
"Sema :Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililosawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yoyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote, wala tusifanyane sisi kwa sisi Miungu Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu" (TMQ 3: 64)

Masoud Msellem 
Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

Tel.: +255 778 8706 09
Pepe: jukwalakhilafah@gmail.com

Hizb ut Tahrir (Mtandao Rasmi) 
www.hizb-ut-tahrir.org
Hizb ut Tahrir (Mtandao Rasmi Afisi Kuu ya Habari)
www.hizb-ut-tahrir.info

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments