Saa 24 zilizopita pamoja na mambo mengine niliona ujumbe katika mtandao wa Wanabidii uliotumwa na mtu mmoja aliyekuwa anamtafuta ndugu yake Raia wa Afrika Kusini aliyekuja Tanzania kupitia Zambia kwa njia ya reli aliyekuwa anaelekea Misri .
Nikaomba kaandika ujumbe kwa wote waliotumiwa ujumbe kuhusu mtu wao na kuomba mawasiliano zaidi ambayo nilipata na jamaa mmoja ndugu Frank Materu alinipitia simu tukaongea kwa kina kidogo kuhusu suala hili , nilimuahidi kulishugulikia ndani ya saa 24 au chini yake baada ya kupata taarifa hiyo .
Kwa kuwa niliona njia alizopitia mpaka kufika Tanzania na nilikuwa na mawasiliano kote huko niliwasiliana na nchi zote alizopita kwa njia ya simu vituoni kuhusu huyu mtu kabla hajafika Tanzania kote kukawa shwari na nikaanza na kuwasiliana na Polisi wa Tanzania , kwanza niliwasiliana na Makao makuu ya Polisi mkoa wa mbeya , askari wa pale anaitwa Bwana Lema akaniomba nimtumie email yenye maelezo yote pamoja na picha za mtuhumiwa na mawasiliano mengine .
Nilituma taarifa zote nilizokuwa nazo kwa wakati huo ingawa kuna nyingine nilihitaji kutoka kwa ndugu wa mtu anayetafutwa ambao walikuwa afrika kusini lakini hiyo haikuninyima fursa ya kutuma zile nilizokuwa nazo kwa wakati huo na mlolongo mzima wa mawasiliano mengine .
Leo asubuhi baada ya saa 10 hivi kupita nilipokea taarifa kwenye anuani ya barua pepe yangu kutoka kwa ndugu wa ROBERTSON kwamba kuna mwili umekutwa sehemu na ndugu wameshajulishwa kinachofuatia ni uchunguzi zaidi utakaofanywa kati ya polisi wa Afrika Kusini na Tanzania kuhusu suala hili .
Sikuishia hapo nilipopata taarifa hiyo tu kuna taarifa nilitakiwa kujiridhisha nazo tena na tena na niliwasiliana na kituo cha Polisi Tazara mkoani mbeya kuhusu suala hili tena badala ya mkoa , Polisi Tazara mkoa wa mbeya wakasema hawana taarifa za tukio lolote kwa abilia wao kuanzia tarehe nilizowatajia na kwamba wao wanaangalia kuanzia mbeya mpaka mafinga lakini kama kuna shida yoyote kwenye reli inayohusu abiria au chochote Tanzania nzima huwa wanapata taarifa lakini hii hawakupokea taarifa ya tukio baya ndani ya mabehewa yao .
Wakaniambia kama abiria amefika usiku na treni huwa wanafuatilia aina ya usafiri anaouchukuwa kwa Tazara , taxi inayomchukuwa na dereva wake anatakiwa kuacha taarifa kuhusu gari yake , yeye mwenyewe na nyingine zitakazohitajika kutuo cha polisi cha Tazara ndio anaruhusiwa kuondoka na abiria , wanafanya hivyo kwa sababu hapo nyuma kuna taxi zilizokuwa zinachukuwa abiria wa kigeni na kwenda kuwapora au kuwafanyia vitu vibaya .
Jioni hii nimepata Ujumbe wa Pongezi tena toka kwa jamaa hawa pamoja na shida iliyotokea kwa ndugu yao .
Ushauri wangu kwa wananchi wenzangu haswa watanzania tusiogope kufanya kazi na vyombo vya usalama haswa jeshi la polisi inapokubidi kufanya hivyo na pale unapotakiwa kutoa taarifa utoe mapema na za ukweli kabisa bila kuonea mtu au watu .
Kwa kufanya hivi tutalisaidia jeshi la polisi kufanya kazi kwa haraka na kwa uhakika na kujihakikishia usalama wetu wa nchi na mali zake sasa na hata siku zijazo .
Pia ni vizuri tuwe na namba muhimu za maeneo ambayo tupo kama ni mkoa , wilaya , makao makuu na nyingine za vyombo hivi au wafanyakazi wake unapopata shida popote ulipo hata kama ni wapi utaweza kusaidiwa mapema na kwa uhakika .
Hongera Jeshi la Polisi lote haswa Mkoa wa Mbeya na Dar es salaam kwa kazi hii nzuri .
Tutaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja
Wembe ni ule ule .
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments