TUNALIMALIZAJE TATIZO LA AJIRA?
Wakati vijana walio wengi( Zaidi ya asilimia50) nchini wakilalamikia tatizo la ukosefu wa ajira, mwanazuoni mahiri, Ibrahim Mohamed Kaduma amekua na maoni tofauti. Kwa mawazo yake anasema kuwa;
Moja kati ya matatizo yanayowakabili vijana ulimwenguni kote ni ukosefu wa ari ya kufanya kazi.
Mara nyingi tunapoongelea juu ya ukosefu wa jira kwa vijana, yatupasa kutambua kwamba kiini cha tatizo ni huo ukosefu wa ari ya kazi unaowapelekea vijana kuchagua kazi fulani fulani tu; na hata wazipatapo kazi walizojichaguli wenyewe, hawazitekelezi kwa ari itakiwayo.
Kwa maneno mengine, vijana wa leo wanataka kufurahia maisha bila kuzalisha chochote kinachoweza kuwa msingi wa huko kufurahia maisha.
Tatizo hilo linakuwa kubwa zaidi kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania. Katika nchi hizo, yale yaliyokwisha kuzalishwa na vizazi vilivyotangulia ni machache sana kulinganisha na nchi zilizoendelea. Ndiyo sababu tunawaona vijana wa nchi changa wanatoroka hata kwa kuhatarish maisha yao kwenda nchi zilizoendelea wakishirikiana na vijana wenzao wa huko kufaidi yale yaliyozalishwa na vizazi vilivyotangulia.
I.M. KADUMA (2010) Maadili ya Taifa na Hatma ya Tanzania: Knowledge Printers, Dar es salaam.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments