Baraza kuu la waislam latoa tamko kuhusu mahakama ya Kadhi.Kwa Jina la Mwenyezi Mungu
Mwingi wa Rehema Mwenye
Kurehemu
JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM
(T)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
17 Mfungo Sita 1436
9 Januari 2014
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI
ZA KIISLAM TANZANIA KUPITIA
VYOMBO VYA HABARI KWA
WATANZANIA WOTE, JUU YA
MUSWADA WA MAREKEBISHO YA
SHERIA MBALIMBALI NA. 02, WA
MWAKA 2014, HUSUSAN KUHUSU
SEHEMU YA MAREKEBISHO
KWENYE SHERIA YA TAMKO LA
SHERIA ZA KIISLAM
Awali ya yote tunapenda kutumia
fursa hii kumshukuru Mwenyezi
Mungu Muumba wa Mbingu, Ardhi
na vilivyomo, na Rehma na Amani
zimfikie Kiongozi wa Ummah
Mtume Muhammad (SAW).
Ndugu wanahabari,
Assalam Alaykum Warahamatul llah
Wabarakatuh.
Tumekuiteni hapa kwa lengo la
kueleza kuhusu Muswada wa
Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
Na. 02, wa mwaka 2014 haswa
kuhusu marekebisho kwenye sheria
ya tamko la Sheria za Kiislamu.
Tunafahamu kuwa kuanzia tarehe
13 hadi 23 Mwezi huu wadau
mbalimbali wataitwa mbele ya
Kamati ya Bunge ya Sheria na
Katiba kwa ajili ya kuwasilisha
mapendekezo yao, Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania
tukiwa sehemu ya wadau muhimu
tunapenda kuwaeleza kuwa
mtiririko wa mchakato wa
marekebisho ya sheria kwa mujibu
wa muswada huu unaokusudia
kutambua Mahakama za Kadhi
Tanzania bara una kasoro kubwa
na kwa dhati unaonesha wazi kuwa
serikali haina nia ya kweli ya
kuunda Mahakama ya Kadhi yenye
hadhi kamili ya kimahakama na
uthabiti wa kuwepo kwake na kuwa
muswada huu ni hadaa nyingine ya
serikali hii ya CCM kwa Waislamu
kwa sababu zifuatazo:-
1. Malalamiko juu ya Mahitaji ya
Mahakama ya Kadhi yana historia
ya kupindishwapindishwa na
serikali hii inayoundwa na CCM.
Kwa mfano katika Ilani ya CCM
mwaka 2005 iliahidi kuanzisha
Mahakama ya Kadhi lakini kwa
ghilba nyingi CCM haikutekeleza
ahadi hiyo baada ya kuingia
madarakani kwa hoja kuwa hili ni
jambo la Kikatiba.
Hata hivyo mchakato wa Katiba
mpya ulipokuja asilimia kubwa ya
maoni ya Waislamu yalihitaji
Mahakama ya Kadhi kuingizwa
ndani ya Katiba, mapendekezo
hayo yalikataliwa na Tume ya Jaji
Warioba kwa hoja kuwa katiba
inayotengenezwa ni ya Muungano
na suala la Mahakama ya Kadhi si
la Muungano hivyo lisubiri wakati
wa kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Waislamu tukavumilia kuisubiri
Katiba ya Tanganyika.
Lakini Bunge Maalum la Katiba
likaikataa Katiba ya Warioba na
kutunga Katiba Mpya Pendekezwa
yenye mambo yote ya Muungano
na yasiyo ya Muungano bila ya
kuingiza Mahakama ya Kadhi kama
ilivyoahidiwa na Tume ya Jaji
Warioba. Bunge la Katiba lililokuwa
linaundwa na wajumbe wengi wa
CCM hawakuona umuhimu wa
kutimiza ahadi yao ya kuweka
Mahakama ya Kadhi katika katiba
pendekezwa na kwa makusudi
Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na
wajumbe wengi wa CCM
walishangilia jambo hili ili hali
wanajua dhahiri kuwa Waislamu
hawakufurahishwa na uamuzi wao
na pia kukiuka Ilani yao na ahadi
kwa Waislamu.
Muswada huu ni sehemu nyingine
ya hadaa kwa Waislamu kwani
badala ya sheria kuanzisha
Mahakama ya Kadhi kama ilivyo
kawaida ya uanzishwaji wa
mahakama zote duniani muswada
huu umeliacha jukumu hilo kwa
taasisi binafsi ili hali Mahakama ya
Kadhi kama zilivyo mahakama
zingine ni sehemu ya chombo cha
dola katika mfumo wa Mahakama
yaani "the Judiciary", hili
limefanywa makusudi kutokana na
kutokuwepo na nia ya dhati ya
Serikali ya CCM kuanzisha na
kuona Tanzania Bara kunakuwa na
Mahakama ya Kadhi madhubuti na
ya ukweli.
2. MUSWADA umempa mamlaka
"Mufti" kuteua makadhi na
kutengeneza kanuni za Uendeshaji
wa Mahakama ya Kadhi ili hali
Mufti sio chombo cha kisheria.
Hakuna sheria inayounda ofisi ya
Mufti isipokuwa uwepo wake
unategemea katiba ya BAKWATA.
Maana yake ni kwamba Mahakama
ya Kadhi uwepo wake utategemea
uwepo wa Katiba ya Bakwata
inayounda ofisi ya Mufti. Kukiwa
na mgogoro wa kikatiba Bakwata
athari yake itaikumba na
Mahakama ya Kadhi. Hakuna
duniani mtu ambaye ofisi yake
haiundwi na sheria kisha sheria
ikampa mtu huyo madaraka ya
kuunda chombo chenye mamlaka
ya kisheria kama mahakama.
Serikali ya CCM inalijua hili lakini
imefanya makusudi kwa kusukumwa
na nia yake ya kutopenda kuona
Waislamu wanakuwa na Mahakama
ya Kadhi ya ukweli iliyo madhubuti.
3. Kama tulivyoeleza hapo juu
MUSWADA umempa Mufti
mamlaka ya kutengeneza kanuni
za uendeshaji wa Mahakama za
Kadhi hili ni jambo la ajabu sana
kwa ofisi ambayo haiundwi na
sheria kuwa na mamlaka ya
kutengeneza kanuni za kuendesha
chombo cha kisheria ambacho ni
Mahakama ya Kadhi. Hili ni jambo
ambalo haliwezekani.
4. Kwa madaraka makubwa
aliyopewa Mufti sheria haielezi ni
nani mwenye mamlaka ya
kumuondoa kadhi na wala
haiweki sifa za kadhi na wala
haiweki vigezo vinavyoweza
kumuondoa kadhi yote hii
inadhihirisha nia ya serikali ya
CCM kuunda Mahakama ya Kadhi
legelege na kiini macho.
5. MUSWADA unaeleza Waziri
anayehusika na mambo ya sheria
kupewa mamlaka ya kutunga
taratibu za kutekeleza hukumu za
Mahakama za Kadhi bila ya
kushauriana na wanazuoni wa
Kiislamu.
Japo katika sehemu ya maelezo ya
muswada Mwanasheria wa Serikali
ameeleza kuwa Waziri atashauriana
na wanazuoni maelezo hayo ni
hewa kwani si sehemu ya sheria.
6. MUSWADA umetoa hiyari kwa
mtu kufungua shauri katika
Mahakama ya Kadhi.
Jambo hili limekusudiwa kuifanya
Mahakama ya Kadhi iwe butu na
kutoa mwanya wa kutokea
mgongano baina ya Mahakama ya
Kadhi na mahakama za kawaida
ikiwa kila upande katika mgogoro
utaamua kufungua shauri katika
mahakama tofauti. Hili
lisingewezekana kama serikali
ingekuwa na nia ya kweli ya
kuunda Mahakama ya Kadhi
madhubuti.
7. MUSWADA kuitaka Mahakama
ya Kadhi ijiendeshe yenyewe:
MUSWAAD huu unaitaka
Mahakama ya Kadhi ijiendeshe
yenyewe badala ya kuendeshwa na
serikali jambo ambalo halijawahi
kutokea sehemu yeyote duniani
chombo kama mahakama
kujiendesha chenyewe.
Mahakama ya Kadhi itafanya
jukumu la serikali katika kutafsiri
sheria za Kiislamu ambazo ni
sheria halali kutumika Tanzania
hakuna mantiki yoyote kwa chombo
hicho kujiendesha chenyewe kama
ambavyo serikali ya CCM inataka
kufanya.
Isitoshe uwepo wa hii Mahakama
ya Kadhi kutaipunguzia serikali
mzigo na msongamano wa kesi
katika mahakama za kawaida jambo
ambalo serikali inapaswa
kugharamia uwendeshwaji wake.
Serikali kukataa kuigharamia hii
Mahakama ya Kadhi ilihali katika
nchi hii upande wa Zanzibar
serikali inaiendesha Mahakama ya
Kadhi kunadhihirisha kuwa kuna
nia ya kuidhoofisha mahakama hii
ishindwe kujiendesha na kuwa na
mahakama isiyokuwa na maana
yoyote.
Zipo mahakama za makundi ya
watu maalumu ambazo
zinaendeshwa kwa pesa za serikali
ambazo ni kodi za Watanzania
wote. Mfano ni kama vile
Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara
n.k. ni kwanini mahakama
itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe
nongwa?
8. UTAFITI unaonyesha kuwa suala
la Mahakama ya Kadhi huletwa kila
unapokaribia Uchaguzi Mkuu bila
ya utekelezaji linazidi kutupa
wasiwasi kwani inaonesha serikali
ya CCM imeshazowea kuwacheza
shere na kuwalaghai Waislamu na
Watanzania kwa ujumla kwa
maslahi yao ya kisiasa. Tabia hii ni
hatari sana kwa mustakabali na
ustawi wa taifa letu.
Hitimisho
Ndugu wanahabari, kwa maelezo
yaliyobainishwa katika taarifa hii,
tunahitimisha kwa kusema:
a) Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
(T) zimeukataa na kupinga
mapendekezo ya marekebisho
kwenye sheria ya tamko la Sheria
ya Kiislam kama lilivyo katika
MUSWADA wa Marekebisho ya
Sheria Mbalimbali na. 02 wa
mwaka 2014, mpaka utakapo
andaliwa upya kwa kuhusishwa
wanazuoni wa Kiislamu, wanasheria
wa Kiislamu waliobobea na kwa
kuzingatia maslahi ya Waislamu na
taifa kwa ujumla na pia Mahakama
ya Kadhi ni lazima iingizwe katika
Katiba ili kuipa uthabiti.
b) Kwa kuwa katiba
inayopendekezwa haitambui
Mahakama ya Kadhi na inapinga
sheria yoyote inayokwenda kinyume
na katiba hiyo ikiwemo Sheria za
Kiislamu kwa kauli moja na kwa
nguvu kubwa Jumuia na Taasisi za
Kiislamu (T) zitawahamasisha
Waislamu na Watanzania kwa
ujumla kuikataa kwa KUPIGA KURA
YA HAPANA katiba
inayopendekezwa muda utakapofika
wa kuipigia kura.
Ndugu waandishi wa habari,
Ahsanteni sana kwa ushirikiano
mliotupa.
Tunawatakia kazi njema katika
ujenzi wa taifa letu.
Kaimu Katibu
-- Mwingi wa Rehema Mwenye
Kurehemu
JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM
(T)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
17 Mfungo Sita 1436
9 Januari 2014
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI
ZA KIISLAM TANZANIA KUPITIA
VYOMBO VYA HABARI KWA
WATANZANIA WOTE, JUU YA
MUSWADA WA MAREKEBISHO YA
SHERIA MBALIMBALI NA. 02, WA
MWAKA 2014, HUSUSAN KUHUSU
SEHEMU YA MAREKEBISHO
KWENYE SHERIA YA TAMKO LA
SHERIA ZA KIISLAM
Awali ya yote tunapenda kutumia
fursa hii kumshukuru Mwenyezi
Mungu Muumba wa Mbingu, Ardhi
na vilivyomo, na Rehma na Amani
zimfikie Kiongozi wa Ummah
Mtume Muhammad (SAW).
Ndugu wanahabari,
Assalam Alaykum Warahamatul llah
Wabarakatuh.
Tumekuiteni hapa kwa lengo la
kueleza kuhusu Muswada wa
Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
Na. 02, wa mwaka 2014 haswa
kuhusu marekebisho kwenye sheria
ya tamko la Sheria za Kiislamu.
Tunafahamu kuwa kuanzia tarehe
13 hadi 23 Mwezi huu wadau
mbalimbali wataitwa mbele ya
Kamati ya Bunge ya Sheria na
Katiba kwa ajili ya kuwasilisha
mapendekezo yao, Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania
tukiwa sehemu ya wadau muhimu
tunapenda kuwaeleza kuwa
mtiririko wa mchakato wa
marekebisho ya sheria kwa mujibu
wa muswada huu unaokusudia
kutambua Mahakama za Kadhi
Tanzania bara una kasoro kubwa
na kwa dhati unaonesha wazi kuwa
serikali haina nia ya kweli ya
kuunda Mahakama ya Kadhi yenye
hadhi kamili ya kimahakama na
uthabiti wa kuwepo kwake na kuwa
muswada huu ni hadaa nyingine ya
serikali hii ya CCM kwa Waislamu
kwa sababu zifuatazo:-
1. Malalamiko juu ya Mahitaji ya
Mahakama ya Kadhi yana historia
ya kupindishwapindishwa na
serikali hii inayoundwa na CCM.
Kwa mfano katika Ilani ya CCM
mwaka 2005 iliahidi kuanzisha
Mahakama ya Kadhi lakini kwa
ghilba nyingi CCM haikutekeleza
ahadi hiyo baada ya kuingia
madarakani kwa hoja kuwa hili ni
jambo la Kikatiba.
Hata hivyo mchakato wa Katiba
mpya ulipokuja asilimia kubwa ya
maoni ya Waislamu yalihitaji
Mahakama ya Kadhi kuingizwa
ndani ya Katiba, mapendekezo
hayo yalikataliwa na Tume ya Jaji
Warioba kwa hoja kuwa katiba
inayotengenezwa ni ya Muungano
na suala la Mahakama ya Kadhi si
la Muungano hivyo lisubiri wakati
wa kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Waislamu tukavumilia kuisubiri
Katiba ya Tanganyika.
Lakini Bunge Maalum la Katiba
likaikataa Katiba ya Warioba na
kutunga Katiba Mpya Pendekezwa
yenye mambo yote ya Muungano
na yasiyo ya Muungano bila ya
kuingiza Mahakama ya Kadhi kama
ilivyoahidiwa na Tume ya Jaji
Warioba. Bunge la Katiba lililokuwa
linaundwa na wajumbe wengi wa
CCM hawakuona umuhimu wa
kutimiza ahadi yao ya kuweka
Mahakama ya Kadhi katika katiba
pendekezwa na kwa makusudi
Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na
wajumbe wengi wa CCM
walishangilia jambo hili ili hali
wanajua dhahiri kuwa Waislamu
hawakufurahishwa na uamuzi wao
na pia kukiuka Ilani yao na ahadi
kwa Waislamu.
Muswada huu ni sehemu nyingine
ya hadaa kwa Waislamu kwani
badala ya sheria kuanzisha
Mahakama ya Kadhi kama ilivyo
kawaida ya uanzishwaji wa
mahakama zote duniani muswada
huu umeliacha jukumu hilo kwa
taasisi binafsi ili hali Mahakama ya
Kadhi kama zilivyo mahakama
zingine ni sehemu ya chombo cha
dola katika mfumo wa Mahakama
yaani "the Judiciary", hili
limefanywa makusudi kutokana na
kutokuwepo na nia ya dhati ya
Serikali ya CCM kuanzisha na
kuona Tanzania Bara kunakuwa na
Mahakama ya Kadhi madhubuti na
ya ukweli.
2. MUSWADA umempa mamlaka
"Mufti" kuteua makadhi na
kutengeneza kanuni za Uendeshaji
wa Mahakama ya Kadhi ili hali
Mufti sio chombo cha kisheria.
Hakuna sheria inayounda ofisi ya
Mufti isipokuwa uwepo wake
unategemea katiba ya BAKWATA.
Maana yake ni kwamba Mahakama
ya Kadhi uwepo wake utategemea
uwepo wa Katiba ya Bakwata
inayounda ofisi ya Mufti. Kukiwa
na mgogoro wa kikatiba Bakwata
athari yake itaikumba na
Mahakama ya Kadhi. Hakuna
duniani mtu ambaye ofisi yake
haiundwi na sheria kisha sheria
ikampa mtu huyo madaraka ya
kuunda chombo chenye mamlaka
ya kisheria kama mahakama.
Serikali ya CCM inalijua hili lakini
imefanya makusudi kwa kusukumwa
na nia yake ya kutopenda kuona
Waislamu wanakuwa na Mahakama
ya Kadhi ya ukweli iliyo madhubuti.
3. Kama tulivyoeleza hapo juu
MUSWADA umempa Mufti
mamlaka ya kutengeneza kanuni
za uendeshaji wa Mahakama za
Kadhi hili ni jambo la ajabu sana
kwa ofisi ambayo haiundwi na
sheria kuwa na mamlaka ya
kutengeneza kanuni za kuendesha
chombo cha kisheria ambacho ni
Mahakama ya Kadhi. Hili ni jambo
ambalo haliwezekani.
4. Kwa madaraka makubwa
aliyopewa Mufti sheria haielezi ni
nani mwenye mamlaka ya
kumuondoa kadhi na wala
haiweki sifa za kadhi na wala
haiweki vigezo vinavyoweza
kumuondoa kadhi yote hii
inadhihirisha nia ya serikali ya
CCM kuunda Mahakama ya Kadhi
legelege na kiini macho.
5. MUSWADA unaeleza Waziri
anayehusika na mambo ya sheria
kupewa mamlaka ya kutunga
taratibu za kutekeleza hukumu za
Mahakama za Kadhi bila ya
kushauriana na wanazuoni wa
Kiislamu.
Japo katika sehemu ya maelezo ya
muswada Mwanasheria wa Serikali
ameeleza kuwa Waziri atashauriana
na wanazuoni maelezo hayo ni
hewa kwani si sehemu ya sheria.
6. MUSWADA umetoa hiyari kwa
mtu kufungua shauri katika
Mahakama ya Kadhi.
Jambo hili limekusudiwa kuifanya
Mahakama ya Kadhi iwe butu na
kutoa mwanya wa kutokea
mgongano baina ya Mahakama ya
Kadhi na mahakama za kawaida
ikiwa kila upande katika mgogoro
utaamua kufungua shauri katika
mahakama tofauti. Hili
lisingewezekana kama serikali
ingekuwa na nia ya kweli ya
kuunda Mahakama ya Kadhi
madhubuti.
7. MUSWADA kuitaka Mahakama
ya Kadhi ijiendeshe yenyewe:
MUSWAAD huu unaitaka
Mahakama ya Kadhi ijiendeshe
yenyewe badala ya kuendeshwa na
serikali jambo ambalo halijawahi
kutokea sehemu yeyote duniani
chombo kama mahakama
kujiendesha chenyewe.
Mahakama ya Kadhi itafanya
jukumu la serikali katika kutafsiri
sheria za Kiislamu ambazo ni
sheria halali kutumika Tanzania
hakuna mantiki yoyote kwa chombo
hicho kujiendesha chenyewe kama
ambavyo serikali ya CCM inataka
kufanya.
Isitoshe uwepo wa hii Mahakama
ya Kadhi kutaipunguzia serikali
mzigo na msongamano wa kesi
katika mahakama za kawaida jambo
ambalo serikali inapaswa
kugharamia uwendeshwaji wake.
Serikali kukataa kuigharamia hii
Mahakama ya Kadhi ilihali katika
nchi hii upande wa Zanzibar
serikali inaiendesha Mahakama ya
Kadhi kunadhihirisha kuwa kuna
nia ya kuidhoofisha mahakama hii
ishindwe kujiendesha na kuwa na
mahakama isiyokuwa na maana
yoyote.
Zipo mahakama za makundi ya
watu maalumu ambazo
zinaendeshwa kwa pesa za serikali
ambazo ni kodi za Watanzania
wote. Mfano ni kama vile
Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara
n.k. ni kwanini mahakama
itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe
nongwa?
8. UTAFITI unaonyesha kuwa suala
la Mahakama ya Kadhi huletwa kila
unapokaribia Uchaguzi Mkuu bila
ya utekelezaji linazidi kutupa
wasiwasi kwani inaonesha serikali
ya CCM imeshazowea kuwacheza
shere na kuwalaghai Waislamu na
Watanzania kwa ujumla kwa
maslahi yao ya kisiasa. Tabia hii ni
hatari sana kwa mustakabali na
ustawi wa taifa letu.
Hitimisho
Ndugu wanahabari, kwa maelezo
yaliyobainishwa katika taarifa hii,
tunahitimisha kwa kusema:
a) Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
(T) zimeukataa na kupinga
mapendekezo ya marekebisho
kwenye sheria ya tamko la Sheria
ya Kiislam kama lilivyo katika
MUSWADA wa Marekebisho ya
Sheria Mbalimbali na. 02 wa
mwaka 2014, mpaka utakapo
andaliwa upya kwa kuhusishwa
wanazuoni wa Kiislamu, wanasheria
wa Kiislamu waliobobea na kwa
kuzingatia maslahi ya Waislamu na
taifa kwa ujumla na pia Mahakama
ya Kadhi ni lazima iingizwe katika
Katiba ili kuipa uthabiti.
b) Kwa kuwa katiba
inayopendekezwa haitambui
Mahakama ya Kadhi na inapinga
sheria yoyote inayokwenda kinyume
na katiba hiyo ikiwemo Sheria za
Kiislamu kwa kauli moja na kwa
nguvu kubwa Jumuia na Taasisi za
Kiislamu (T) zitawahamasisha
Waislamu na Watanzania kwa
ujumla kuikataa kwa KUPIGA KURA
YA HAPANA katiba
inayopendekezwa muda utakapofika
wa kuipigia kura.
Ndugu waandishi wa habari,
Ahsanteni sana kwa ushirikiano
mliotupa.
Tunawatakia kazi njema katika
ujenzi wa taifa letu.
Kaimu Katibu
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments